Kocha wa Ivory Coast |
KOCHA wa timu ya taifa ya Ivory Coast Herve Renard amedai kuwa,
wapinzani wao Algeria walikuwa wazuri zaidi yao licha ya kuwafunga bao 3-1
katika mchezo wa robo fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika.
Renard ambaye aliwahi kuipa Zambia ubingwa wa michuano hiyo
alisema kuwa, kikosi chake jana usiku kilikuwa dhaifu licha ya ushindi huo
ulioiwezesha kutinga hatua ya nusu fainali ya mashindano hayo.
Washindi wa mchezo huo ndio walikuwa wa kwanza kupata bao
lililowekwa kimiani na mchezaji mpya wa Manchester City Wilfried Bony, ambaye
pia ndiye aliyefunga la pili baada ya Mualgeria El Arbi Hillel Soudani kusawazisha.
Gervinho aliihakikishia Ivory Coast ushindi baada ya kufunga bao
la tatu katika dakika za majeruhi katika mchezo huo uliofanyika jijini hapa na
kuihakikishia timu hiyo nafasi ya kusonga mbele.
Renard alisema kuwa wapinzani wao hao kutoka Afrika ya Kaskazini
walikuwa wazuri, lakini walishindwa kutumia nafasi zao vizuri.
"Kwa upande wa soka, mbinu, Algeria walikuwa bora zaidi yetu,
" alisema Renard alipozungumza na waandishi wa habari mara baada ya mchezo
huo.
Timu hiyo sasa itavaana na DR Congo walioiondosha Congo kwa mabao 4-2, timu nyingine iliyofuzu nusu fainali ni Ghana iliyoicharaza Guinea kwa mabao 3-0 na sasa watacheza na wenyeji Guinea ya Ikweta keshokutwa.
Naye Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Algeria Christian Gourcuff aliunga
mkono maneno ya mwenzake, ambapo alisisitiza kuwa timu iliyoshinda haikuwa
bora.
"Hii sio timu bora iliyoshinda. Kwa upande wa mchezo,
tulicheza vizuri lakini bahati haikuwa yetu, " alibainisha Gourcuff.
"Wachezaji wa Ivory Coast hawakupata nafasi nyingi.
Hawakustahili kushinda."
Gourcuff pia alitupia lawama ubora wa kiwanja, na kusema kuwa
lilikuwa kosa lao kukubali kufungwa na Ghana baada ya kukubali bao la dakika za
mwisho na kumaliza wa pili katika Kundi C kwani wangeshinda wangekuwa wa kwanza
na wangeikwepa Ivory Coast katika robo fainali.
"Lakini ikiwa tumecheza mechi 10, lakini haujafungwa mara 10,
ni wazi sisi ni timu bora…”
No comments:
Post a Comment