STRIKA
USILIKOSE
Sunday, January 19, 2014
Yanga sasa kumaliza na Simurq PIK kesho Uturuki
Na Baraka Kizuguto, Uturuki
MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara Young Africans kesho jumatatu saa 8 mchana kwa saa za nchini Uturuki sawa na saa 9 kamili kwa saa za Afrika Mashariki itashuka dimbani kucheza mchezo wake wa mwisho wa kirafiki dhidi ya timu ya Simurq PIK inayoshiriki Ligi Kuu nchini Azerbajain katika viwanja vya Side Manavgat.
Kocha mkuu wa Young Africans mholanzi Hans Van Der Plyum amesema watautumia mchezo huo kama sehemu ya mwisho ya maandalizi ya kujianda na Ligi Kuu ambayo inatarajiwa kuanza mwishoni mwa wiki ijayo ambapo watoto wa jangwani watafugua dimba dhidi ya Ashanti United uwanja wa Taifa.
Mchezo wa kesho utakua mgumu pia, kwani timu ya Simurq PIK ina wachezaji wazuri ambao wanatoka sehemu mbali mbali dunianina ipo katika nafasi ya tano katika msimamo wa Ligi Kuu nchini kwao, hivyo nadhani kitakua kipimo kizuri cha mwisho kabla ya kurejea nchini Tanzania
Akiongelea kikosi chake mara baada ya mazoezi ya asubuhi, Hans amesema anashukuru mungu maendeleo ya timu ni mazuri, mabadiliko yapo na wachezaji wanaonekana kumuelewa hivyo anaamini kadri siku zinavyokwenda timu itakua katika kiwango kizuri zaidi.
"Nimeshashuhudia michezo miwili mmoja tukishinda 2-0 dhidi ya timu ya Altay SK Lidi Daraja la pili Uturuki na jana tukitoka sare ya 0-0 dhidi ya timu ya KS Flumartari ya Ligi Kuu Albania, kwa kweli nawapongeza vijana wanaonyesha kweli wanajua wajibu wao na kucheza kwa kufuata maelekezo ya walimu" alisema Hans.
Aidha Hans amesema ni jambo njema timu imecheza jumla ya michezo mitatu, ikishinda miwili na kutoka sare mchezo mmoja, huku ikifunga mabao 5 na kutokuruhusu nyavu zake kutikisika hii yote inayonyesha timu imeiva tayari kwa mashindano yanayotukabili.
Mpaka sasa hakuna mchezaji majeruhi hata mmoja kufuatia kiungo Hassan Dilunga kupona malaria na kuungana na wenzake katika mazoezi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment