* Yaungana na Mali wakiwaacha wenyeji wakishangaa
* Uganda kibaruani kwa Morocco leo
MABINGWA wa Afrika, Nigeria jana iliwaduwaza wenyeji wa michuano ya CHAN 2014 Bafana Bafana ya Afrika Kusini baada ya kuwakandika mabao 3-1 na kuitupa nje kwenye michuano hiyo, huku wenyewe wakifuzu robo fainali kutoka kundi A.
Nigeria iliyoanza kwa kipigo cha mabao 2-1 kutoka Mali, ilibashiriwa ingekuwa na wakati mgumu katika mechi hiyo ya jana dhidi ya wenyeji, lakini walifanya kisichotarajiwa kwenye uwanja wa Cape Town baada ya kupata ushindi huo uliowafanya wakamate nafasi ya pili.
Mabao mawili ya Uzoenyi katika dakika ya 22 na jingine la 64 na lile la mkwaju wa penati kupitia kwa Ede iliivusha Nigeria hatua ya mtoano sawia na vinara wa kundi hilo la A, Mali ambayo iliichapa Msumbiji mabao 2-1 na kufikisha pointi saba.
Bao la wenyeji lilifungwa na kinara wa mabao katika michuano hiyo Bernard Parker kwa mkwaju wa penati na kumfanya asfikishe mabao manne mpaka sasa.
Katika mchezo wa Msumbiji na Mali ambao ulichezwa muda mmoja na pambano la Nigeria na Afrika Kusini, Msumbiji waliokuwa wa kwanza kuaga michuano hiyo walianza kupata bao dakika ya 38 kupitia kwa Josemar aklimalizia kazi ya Mario..
Hata hivyo Sidibe alisawazisha bao hilo dakika tatu tangu kuanza kwa kipindi cjha pili kabla ya
Ibraouma Traore kufunga bao la ushindi dakika za nyongeza za pambano hilo na kuivusha Mali hadi robo fainali.
Michuano hiyo0 itaendelea leo kwa michezo ya kundi B ambapo timu nyingine mbili za kutinga robo fainali zitafahamika ambapo, Uganda the Cranes wanaoongoza kwa sasa katika kundi hilo watavaana na Morocco, huku Zimbabwe watapepetana na Burkina Faso.
No comments:
Post a Comment