Sami Khedira |
KLABU ya Chelsea
imepata nguvu mpya ya mapambano ya kupata saini ya Sami Khedira kufuatia
wakala wake kudai kuwa hakuna mazungumzo yoyote yaliyofikiwa mpaka sasa
na Arsenal.
Meneja
wa 'The Blues'
Jose Mourinho amefanikisha usajili wa mlinzi wa kushoto Filipe Luis
akitokea Atletico Madrid kwa ada ya uhamisho ya pauni milioni £18 na
sasa anajipanga kwa ajili ya kiungo wa kimataifa wa Ujerumani Khedira.
Hapo
kabla ilikuwa imefahamika kuwa Arsenal
imekamilisha dili la uhamisho wa kiungo huyo mwenye umri wa miaka 27
kwa ada ya pauni milioni £20, lakini walikwama kufikia makubaliano ya
mshahara wake wa wiki ambao nyota huyo alikuwa akitaka zaidi ya pauni
£180,000.
Amekaririwa wakala wa Khedira, Jorg Neubauer akisema
‘Hatuko kwenye mazungumzo na Arsenal. Sidhani kama ada itakubalika, vinginevyo wange kwisha kunipatia taarifa.’
Khedira
amekuwa akimpendeza Mourinho tangu wakati huo akiwa bosi wa Real na
inaelezwa kuwa huenda Mourinho akamvuta Stamford Bridge.
Usajili: Bosi wa Chelsea Jose Mourinho amesha msajili Diego Costa na Filipe Luis
Wakati hayo yakiwa hivyo, Chelsea imethibitisha makubaliano na mlinzi wa kushoto wa Atletico Fillipe Luis.
Mlinzi
huyo mwenye umri wa miaka 28 atakamilisha uhamisho wake baada ya
kufanikisha kipimo cha afya na makubaliano ya maslahi binafsi.
Usajili
wa Mourinho unaendelea akiwa bado katika ushawishi kwa Khedira,
matumaini yake ya kumsajili Antoine Griezmann aliyethaminishwa kwa pauni
£20 na klabu yake ya Real Sociedad huenda yakagonga mwamba kufuatia
upinzani mkubwa kutoka kwa vilabu vya Monaco na Liverpool.
No comments:
Post a Comment