STRIKA
USILIKOSE
Sunday, July 28, 2013
Uchaguzi Mkuu wa BFT sasa Oktoba 26 Morogoroooo!
UCHAGUZI Mkuu wa Shirikisho la Ngumi za Ridhaa Tanzania (BFT) ambao ulikwama kufanyika Julai 7 mwaka huu jijini Mwanza sasa utafanyika Oktoba 26 mjini Morogoro.
Kwa mujibu wa taarifa iiyotolewa na Katibu Mkuu wa BFT, Makore Mashaga kwa MICHARAZO ni kwamba uamuzi wa tarehe hiyo na eneo jipya la kufanyia uchaguzi huo ulitolewa juzi na Kamati ya Utendaji ya shirikisho hilo iliyokutana jijini Dar es Salaam na kuudhuriwa na viongozi wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT).
Uchaguzi huo ulikwama kufanyika kama ulivyopangwa kutokana na idadi ndogo ya wagombea waliojitokeza, nafasi nyingine zikikosa kabisa wagombeaji na idadi ndogo ya wapiga kura iliyoshindw kufikia kolamu.
Mashaga alisema kuwa baada ya kamati kukaa chini na kujadili cha kufanya hatimaye iliamriwa uchaguzi huo sasa upafanyike Oktoba kutoa muda wa kujitokeza kwa wagombea huku wakipewa maelekeo na BMT wanahyotakiwa kutekeleza ndani ya siku 90.
Katibu huyo alisema maelekezo waliyopewa ni pamoja na kurekebisha katiba yao ili kulingana na maagizo ya msajili wa vyama vya michezo na ile a Shirikisho la Ngumi la Kimataifa (AIBA).
Pia kuhakiki uhai wa wanachama wake na kusajili wengine kulingana na maekelezo ya katiba ya BFT pamoja na kuhakikisha BFT inajamasisha wadau kuijitokeza kuwania uongozi katika uchaguzi huo.
"Baada ya maamuzi hayo ni kwamba sasa BFT tunaanza upya mchakato wa uchaguzi huo na kwamba safari hii utafanyika Morogoro Oktoba 26," alisema.
Uongozi wa sasa BFT uliingia madarakani Machi 2009 baada ya waliokuwa viongozi wa shirikisho hilo chini ya akina Shaaban Mintanga kujiuzulu kutokana na kashfa ya dawa za kulevya iliwahusisha mabondia waliokamatwa Mauritius walipoenda kushiriki michuano ya Afrika.
Taarifa rasmi ya BFT hiyo hapo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment