Coastal Union yazidi kutisha, yainyuka Simba kidude
TIMU ya soka ya Coastal Union ya Tanga imeendelea kuvitisha vigogo vya soka nchini ikiwa ni mwezi mmoja kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2013-2014 baada ya jioni hii kuikwanyua Simba kwa bao 1-0 katika mechi ya kirafiki.
Ushindi huo ni wa pili mfululizo kwa mabingwa hao wa zamani wa soka nchini baada ya katikati ya wiki kuutafuna mfupa uliovishinda vigogo hivyo kwa URA baada ya kuwalaza Waganda hao bao 1-0.
Kabla ya kipigo hicho URA iliilaza Simba mabao 2-1 na kukaribia kuiadhiri Yanga kabla ya mabingwa hao wa kandanda nchini kuchimoa dakika za lala salama na kuambulia sare ya mabao 2-2.
Pambano la leo lililochezwa kwenye uwanja wa Mkwakwani Tanga ilishuhudiwa hadi wakati wa mapumziko kukiwa hakuna mbabe yeyote baada ya timu zote kutoshanga nguvu ya kutofungana.,
Hata hivyo katika kipindi cha pili Coastal walionyesha ilivyopania msimu ujao kwa kuwakimbiza Simba na kujipatia bao pkee lililowekwa kimiani na mchezaji wao mpya toka Kenya,
Crispian Odula Odwenye aliyefunga katika dakika 54.
Hicho ni kipigo kingine kwa Simba katika mechi zake za karibu za kirafiki za kujipima nguvu na inamfanya kocha wake, King Abdallah Kibadeni kurekebisha mapema kikosi chake kabla ya ligi.
No comments:
Post a Comment