Ronaldo alishangilia moja ya mabao yake jana |
Akiendelea kufunga |
jamaa huyu balaa! |
Akishangilia na wenzake ushindi wa nyumbani Santiago Bernabeu |
Hat trick hiyo ni ya 23 kwa Mreno huyo na kumfanya kuwa mchezaji anayeongoza kwa hat trick nyingi katika La Liga kwa sasa, licha ya kukamata nafasi ya 9 ya wachezaji wenye magoli mengi katika ligi hiyo akiwa nyuma ya mabao 53 dhidi ya 'hasimu' wake, Lionel Messi mwenye mabao 253.
Mabao hayo yamemfanya mchezaji huyo kufikisha mabao 200 katika mechi 178 za La Liga kwa misimu wake wa sita nchini humo na pia ni bao la 23 katika mechi 13 za msimu huu, kiasi ambacho ukichukua mabao ya hasimu wake na ya mshambuliaji mwingine nyota wa Barecelona, Neymar hayafikii idadi hiyo ya mabao.
Ronaldo ambaye hakuwepo katika mechi ya Kombe la Mfalme wakati Real Ikishinda mabao 5-0 dhidi ya Cornellà, alianza kuandika bao la kwanza kwa mkwaju wa penati katika dakika ya 36.
Katika kipindi cha pili mkali huyo aliongeza tena mabao mawili katika dakika ya 65 na na 81 alipomaliza kazi nzuri ya Marcelo na kuifanya Real kuzidi kujichimbia kileleni na kuikimbia Atletico.
Ushindi huo umeifanya Real kufikisha pointi 36 wakati wapinzani wao ambao pia ndio mabingwa watetezi wakiwa na 32.
Katika mechi nyingine ya ligi hiyo jana Athletico Bilbao ililala nyumbani kwa bao 1-0 dhidi ya Cordoba na leo kutakuiwa na michezo mingine kadhaa likiwamo pambano la Barcelona dhidi ya wapinzani wao wa Jimbo la Cataluna, Espaniola.
Wakali wa Hat Trick wa Muda wote La Liga Hawa Hapa:
23- CRISTIANO RONALDO
22- Di Stéfano and Zarra
20- Messi
19- Mundo
16- César
13 Lángara
No comments:
Post a Comment