KOCHA wa klabu ya
Manchester United, Louis Van Gaal amehakikishiwa kupewa fedha za kufanya usajili kwenye kipindi cha Majira ya Kiangazi ili kuimarisha kikosi chake.
Uongozi wa klabu hiyo wamemueleka LVG kuwa pesa siyo tatizo
kama akiamua kuimarisha kikosi chake katika kipindi cha majira ya
kiangazi.
Van Gaal alitumia kitita cha paundi milioni 150 katika majira
ya kiangazi, ukiwemo usajili uliovunja rekodi Uingereza wa paundi
milioni 59.7 kwa ajili ya Angel Di Maria lakini bado wanaburuzwa na
vinara Chelsea kwa tofauti ya alama 11 katika msimamo wa Ligi Kuu.
Kiungo wa ulinzi Kevin Strootman na mabeki Mats Hummels na Diego Godin
wote wako katika rada za United.
Hata hivyo, Ofisa Mkuu wa United Ed
Woodward tayari ameshweka wazi kuwa hatataka kuchukua mchezaji kwa mkopo
katika kipindi cha usajili wa dirisha dogo Januari.
Woodward
alibainisha mwezi uliopita kuwa tayari wana wachezaji waliowalenga kwa
ajili ya usajili ujao wa majira ya kiangazi ila yoyote atakayeweza
kupatikana Januari watafanya mipango ya kumchukua.
No comments:
Post a Comment