WATU 7 wamenusurika kupoteza maisha baada ya ndege waliyokuwa
wakisafiria kuanguka na maeneo ya Longido Mkoani Arusha juzi Jumanne.
Duru za Jeshi la Polisi
mkoa wa Arusha zimesema majira ya saa 8 za mchana katika kijiji cha Merugwayi
ndege aina ya CESS iliyokuwa na namba za usajili TN/4206 ikiwa na marubani
wawili ilipata ajali.
Taarifa hiyo ya Jeshi la
Polisi imetaja chanzo cha ajili hiyo kuwa ni upepo mkali uliosababisha ishindwe
kupaa katika uwanja wa ndege wa Merugwayi umbali wa mita 120 na kuanguka.
Habari zaidi zinasema
ndege hiyo iliondoka Arusha majira ya saa 2 za asubuhi kuelekea wilayani
Ngorongoro na baadaye ilirudi tena Arusha ikiwa na Abiria watano ilipofika
katika uwanja huo ilishuka kwa ajili ya kuchukua mgonjwa na ilipojaribu kuruka
ilishindwa, na kupoteza mwelekeo.
Marubani waliokuwemo
katika ndege hiyo ni Jaffer Shakir (23) na Patten Patrick (65).
Hata hivyo Kaimu Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Arusha ACP Japhet Lusingu amewataja majeruhi kuwa Nalepo
MamaSita (38), Anna Laizer (21), Naninkoi Laizer (7), Benson Mukoya (28),
Krizosto Malima (30).
Rubani wa ndege hiyo
Jaffer Shakir ameumia vibaya sehemu za usoni
na amelazwa katika Hospitali ya Selian, Jijini Arusha kwa matibabu zaidi huku
wengine wakiruhusiwa.
Jaizmalaleo
No comments:
Post a Comment