STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, May 21, 2013

Stars yaingia kambini bila akina Samatta


TIMU ya taifa ya soka (Taifa Stars) jana jioni ilianza rasmi kambi yake jijini Dar es Salaam kujiandaa kwa ajili ya mechi ya marudiano ya Kundi C dhidi ya timu ya taifa ya Morocco (Simba wa Atlasi) itakayopigwa Juni 8 mwaka huu kuwania kufuzu kushiriki fainali zijazo za Kombe la Dunia zitakazofanyika Brazili 2014.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura alisema kuwa kikosi kilichoingia kambini jana kinaanza mazoezi rasmi leo jijini Dar es Salaam na kinawakosa washambuliaji wawili, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu, ambao wako na timu yao ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
"Wachezaji wote walioitwa na kocha (Kim Poulsen) isipokuwa Samatta na Ulimwengu wanaingia kambini ni leo (jana) jioni kuanza kambi ya Stars na kesho (leo) wataanza rasmi mazoezi kabla ya safari ya Ethiopia ambako Stars itacheza mechi ya kirafiki dhidi ya timu ya taifa ya Sudani Juni 2," alisema Wambura.
 Alisema kuwa Samatta na Ulimwengu wameshindwa kuungana na kikosi cha Mdenmark Poulsen kwa sababu bado wanahitaji kwenye kikosi cha TP Mazembe kinachoshiriki Kombe la Shirikisho barani Afrika na kwamba wataungana na Stars mjini Marrakech, Morocco Juni 3.
Katika mechi ya kwanza iliyochezwa Machi 24 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Stars mabyo kwenye kundi hilo imepangwa pia na timu za Ivory Coast na Gambia, ilishinda 3-1.
Ivory Coast ndiyo wanaongoza kundi hilo wakikwa na pointi 7 wakifuatwa na Taifa Stars wenye pointi 6 wakati Morocco wanakamata nafasi ya tatu baada ya kujikusanyia pointi mbili huku Gambia wakishika mkia baada ya kuambulia pointi moja tu katika mechi zote tatuy ambazo kila timu kwenye kundi hilo imeshacheza.

No comments:

Post a Comment