Mbeya City wamemaliza kwa ushindi nyumbani dhidi ya Polisi |
Polisi wameenda na maji |
Yanga walioendelea kutoa takrima kwa timu pinzani |
Azam walimaliza kwa kishindo nyumbani |
JKT Ruvu licha ya kichaapo cha Simba wamenusuurika kushuka draja |
Ndanda wamepona baada ya kuilaza Yanga |
Simba waliomaliza ligi kwa kishindo kwa kuiparua JKT Ruvu |
Prisons wameponea chupuchupu |
Mtibwa wamemaliza kwa kichapo nyumbani mbele ya Coastal Union |
Ruvu inayonolewa na kocha Mkenya Tom Olaba ilikuwa ugenini Uwanja wa Kambarage
mkoani Shinyanga na kujikuta ikipokea kipigo cha bao 1-0 na wenyeji wao Stand
United ambayo ushindi huo umeifanya kufikisha pointi 31 katika nafasi ya 10.
Polisi Moro iliyopanda kucheza Ligi Kuu msimu huu, ilikubali kipigo cha
bao 1-0 kutoka kwa Mbeya City na kujikuta ikirudi ilipotoka na hiyo inatokana
na mwenendo wa kusuasua tangu kuanza kwa msimu huu ikiwemo uongozi kubadilisha
makocha mara kwa mara.
Polisi Moro ndiyo timu pekee msimu huu ambayo imefundishwa na makocha
watatu, ilianza na Adolf Rishard 'Adolf' kisha ikamfukuza na kumchukua Amri Said,
ambaye naye aliamua kujiondoa na nafasi yake kuchukuliwa na John Tamba, lakini
hadi siku jana walijikuta wakiburuza mkia wakiwa na pointi zao 25 katika mechi
26 walizocheza.
Katika uwanja wa Nang'wanda Sijaona mkoani Mtwara, Mabingwa wapya wa
msimu huu Yanga waliendelea kuonja shubiri baada ya kupoteza mchezo huo kwa
kufungwa bao 1-0 na wenyeji Ndanda FC, Wakati kwenye Uwanja wa Azam Complex
wenyeji Azam walitoka sare ya bila kufungana na Mgambo JKT ya Tanga.
Kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza kocha, Mbwana Makatta,
alifanikiwa kuiokoa timu ya Tanzania Prisons isishuke daraja msimu huu baada ya
kuilazimisha sare ya bila kufungana na Kagera Sugar aliyomaliza nafasi ya sita
ikiwa na pointi 32, huku sare hiyo ikiwasaidia maafande hao kufikisha pointi 29
na kuepuka janga la kurudi kushuka daraja la kwanza msimu ujao.
Katika uwanja wa Manungu Turiani, Mtibwa Sugar ililala nyumbani kwa
kufungwa mabao 2-1 na Coastal Union ya Tanga na matokeo hayo kuifanya timu hiyo
iliyokuwa na kipindi kigumu licha ya kunza msimu huu vizuri kumaliza nafasi ya
saba msimu huu ikiwa na pointi 31 huku Wagosi wa Kaya wakimaliza nafasi ya tano
wakiwa na pointi 34.
Msimamo wa mwisho wa Ligi Kuu ya Bara:
P W D L F A Pts
1. Yanga 26 17 4 5 52 18 55
2. Azam 26 13 10 3 36 18 49
3. Simba 26 13 8 5 38 19 47
4. Mbeya City26 8 10 8 22 22 34
5. Coastal 26 8 10 8 21 25 34
6.Kagera 26 8 8 10 22 26 32
7. Mtibwa 26 7 10 9 25 25 31
8. JKT Ruvu 26 8 7 11 20 25 31
9. Ndanda 26 8 7 11 21 29 31
10.Stand 26 8 7 11 23 34 31
11. Prisons 26 5 14 7 18 22 29
12. Mgambo 26 8 5 13 18 28 29
13. Ruvu 26 7 8 11 16 29 29
14. Polisi Moro26 5 10 11 16 27 25
Matokeo:
JKT Ruvu v Simba (1-2)
Mtibwa Sugar v Coastal Union (1-2)
Stand Utd v Ruvu Shooting(1-0)
Mbeya City v Polisi Moro (1-0)
Kagera Sugar v Prisons (0-0)
Ndanda v Yanga (1-0)
Azam v Mgambo JKT (0-0)
WAFUNGAJI:
17- Simon Msuva (Yanga)
14- Amissi Tambwe (Yanga)
11- Abaslim Chiidiebele (Stand Utd)
10-Didier Kavumbagu (Azam)
Rashid Mandawa (Kagera Sugar)
Emmanuel Okwi (Simba)
9- Malimi Busungu (Mgambo)
8- Samuel Kamuntu (JKT Ruvu)
Ibrahim Ajibu (Simba)
Ame Ali (Mtibwa)
7-Rama Salim (Coastal)
6- Kipre Tchetche (Azam)
Danny Mrwanda (Yanga)
Heri Mohammed (Stand)
5- Jacob Massawe (Ndanda)
Yahya Tumbo (Ruvu)
Atupele Green (Kagera)
Mussa Mgosi (Mtibwa)
Nassor Kapama (Ndanda)
4- Ally Shomari (Mtibwa)
Themi Felix (Mbeya City)
Said Bahanuzi (Polisi Moro)
Frank Domayo (Azam)
Mrisho Ngassa (Yanga)
Kpah Sherman (Yanga)
Gaudence Mwaikimba (Azam)
Andrey Coutinho (Yanga)
Ramadhani Singano (Simba)
3- Dan Sserunkuma (Simba)
Elias Maguli (Simba)
Ally Nassor (Mgambo)
Raphael Alpha (Mbeya City)
Aggrey Morris (Azam)
Paul Nonga (Mbeya City)
NB:WAKILISHI WA NCHI, ZILIZOSHUKA DARAJA
Msimamo wa mwisho wa Ligi Kuu ya Bara:
P W D L F A Pts
1. Yanga 26 17 4 5 52 18 55
2. Azam 26 13 10 3 36 18 49
3. Simba 26 13 8 5 38 19 47
4. Mbeya City26 8 10 8 22 22 34
5. Coastal 26 8 10 8 21 25 34
6.Kagera 26 8 8 10 22 26 32
7. Mtibwa 26 7 10 9 25 25 31
8. JKT Ruvu 26 8 7 11 20 25 31
9. Ndanda 26 8 7 11 21 29 31
10.Stand 26 8 7 11 23 34 31
11. Prisons 26 5 14 7 18 22 29
12. Mgambo 26 8 5 13 18 28 29
13. Ruvu 26 7 8 11 16 29 29
14. Polisi Moro26 5 10 11 16 27 25
Matokeo:
JKT Ruvu v Simba (1-2)
Mtibwa Sugar v Coastal Union (1-2)
Stand Utd v Ruvu Shooting(1-0)
Mbeya City v Polisi Moro (1-0)
Kagera Sugar v Prisons (0-0)
Ndanda v Yanga (1-0)
Azam v Mgambo JKT (0-0)
WAFUNGAJI:
17- Simon Msuva (Yanga)
14- Amissi Tambwe (Yanga)
11- Abaslim Chiidiebele (Stand Utd)
10-Didier Kavumbagu (Azam)
Rashid Mandawa (Kagera Sugar)
Emmanuel Okwi (Simba)
9- Malimi Busungu (Mgambo)
8- Samuel Kamuntu (JKT Ruvu)
Ibrahim Ajibu (Simba)
Ame Ali (Mtibwa)
7-Rama Salim (Coastal)
6- Kipre Tchetche (Azam)
Danny Mrwanda (Yanga)
Heri Mohammed (Stand)
5- Jacob Massawe (Ndanda)
Yahya Tumbo (Ruvu)
Atupele Green (Kagera)
Mussa Mgosi (Mtibwa)
Nassor Kapama (Ndanda)
4- Ally Shomari (Mtibwa)
Themi Felix (Mbeya City)
Said Bahanuzi (Polisi Moro)
Frank Domayo (Azam)
Mrisho Ngassa (Yanga)
Kpah Sherman (Yanga)
Gaudence Mwaikimba (Azam)
Andrey Coutinho (Yanga)
Ramadhani Singano (Simba)
3- Dan Sserunkuma (Simba)
Elias Maguli (Simba)
Ally Nassor (Mgambo)
Raphael Alpha (Mbeya City)
Aggrey Morris (Azam)
Paul Nonga (Mbeya City)
NB:WAKILISHI WA NCHI, ZILIZOSHUKA DARAJA
No comments:
Post a Comment