STRIKA
USILIKOSE
Sunday, May 10, 2015
Rasmi Kagame Cup kupigwa Dar kuanzia Julai 11-Agosti 02
HATIMAYE imefahamika kuwa, michuano ya Kombe la Kagame kusaka Bingwa wa Afrika Mashariki na Kati kwa ngazi za klabu itapigwa Tanzania.
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limekubali kuwa wenyeji wa michuano ya Kombe la Kagame baada ya kutafakari kwa kina.
Baraza la Vyama vya Soka kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) waliiteua Tanzania kuandaa michuano hiyo, lakini uongozi wa TFF, ulisema ungekutana kujadili kabla ya kutoa tamko.
Hata hivyo kwa mujibu wa taarifa ya shirikisho hilo ilitolewa jana kwa vyombo vya habari TFF imethibitisha kuwa wamekubali kuandaa michuano hiyo na kutangaza kwamba itaanza kutimua vumbi lake kuanzia Julai 11 na kufikia tamati Agosti 2, mwaka huu.
TFF imeweka bayana kwamba Cecafa ndiyo itakayotangaza timu shiriki pamoja na ratiba nzima ya michuano hiyo ambayo mara ya mwisho kufanyika Tanzania ilikuwa mwaka 2012 ambapo Yanga ilitwaa taji kwa mara ya pili mfululizo kwa kuilaza Azam katika fainali iliyopigwa Uwanja wa Taifa. Mwaka mmoja nyuma yaani 2011 Yanga ilitwaa tena taji michuano ilipochezwa jijini Dar es Salaam kwa kuilaza Simba bao 1-0.
Bingwa mtetezi wa michuano hiyo kwa sasa ni wababe wa Azam, El Merreikh ya Sudan ambao walitwaa taji katika fainali zilizochezwa mwaka jana mjiji Kigali, Rwanda baada ya kuilaza APR bao 1-0.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment