STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, May 10, 2015

Kampuni ya Bima ya UAP yatoa elimu kwa wakulima Kanda ya Ziwa

Picha tofauti zinaoonyesha  Pamba zilizokuwa zimehifadhiwa katika ghla na kuungua na chini ni maafisa wa kampuni ya Bima UAP wakiwa na Meneja wa Kiwanda cha JIELONG Holdings Tanzania LTD Kiki Huwa Xu (kushoto).

Na Renatha Msungu
WANANCHI wa mkoa wa Shinyanga wamenufaika na elimu ya kutunza maghala ya chakula na pamba iliotolewa na kampuni ya bima ya UAP kwa ajili ya
kuzuia wasipatwe na majanga ya moto.
Elimu hiyo imetolewa kwa wakazi wa mkoa huo, baada ya mmiliki wa ghala la Jielong Holdings, Kiki Jielong kuunguliwa na ghala lake la pamba
lililopo nje kidogo ya mji wa Shinyanga, kwenye hafla ya kukabidhi hundi kwa ajii ya fidia hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Shinyanga jana, Meneja Maendeleo wa biashara wa UAP Raymond Komanga, alisema hii ni moja ya
faida ya kujiunga na bima ya nyumba ambayo inasaidia kutoa fidia ya hasara inayopatikana kwenye maghala kama hilo la Jielong.
Komanga alisema kutokana na hilo wameamua kutoa elimu kwa wafanya biashara na wamiliki wa maghala mkoani humo ili waweze kujikinga na athari ambazo  zinaweza kutokea wakati wowote.
Alisema wamekuwa wakipata kesi nyingi za aina hiyo na kuzitatua tu kwa wale ambao wamejiunga na bima kwa ajili ya kujikinga na majanga yanayotokea katika sehemu zao za kazi.
Alisema wameanza mkoani Shinyanga na wataendelea katika mikoa mingine ili kutoa elimu ya kujikinga na majanga mbalimbali ya moto na mengine yanayowatokea kila kukicha.
Alisema wananchi wengi hawajakata bima jambo ambalo linawapa shida mara baada ya kupata matatizo ya kuunguliwa na nyumba na kushindwa
kuzirejesha kwa wakati.
Kwa upande wake mmiliki wa ghala hilo na ambaye ni meneja Utawala wa kampuni ya Jielong, alisema wanaishkuru UAP kutokana na kuwarejeshea
fedha hizo haraka baada ya kupata ajali hiyo ya moto katika ghala lao.
Alisema wao ni wanachama wa muda mfupi lakini walipotoa taarifa mara moja watu wa bima walijitokeza na kuwasaidia kufidia gharama
zilizoungua katika ghala hilo la kuhifadhia pamba.
Akielezea chanzo cha moto ndani ya ghala hilo alisema umetokana na joto la ndani ya ghala baada ya bidhaa zilizopo ndani kubanana na kukosa hewa na kusababisha pamba kuwaka moto.
Alisema moto huo ulisambaa kwa kasi kubwa kutokana na kwamba pamba inashika moto kwa haraka kuliko kitu kingine.
Alisema anawashauri wafanya biashara ambao hawajakata bima wajitokeze kwenda kukata bima hiyo kwa kuwa ina manufaa makubwa sana, hasa wakati wa matatizo.
Meneja madai wa UAP Emmanuel Michael aliwataka wafanya biashara kuwa makini na bidhaa zao ili kuepusha majanga ya moto yasiwatokee.
Alisema wafanya biashara wengi wamekuwa wazembe kujifunza elimu ya kujikinga na majanga ya moto ambayo huwapatia hasara kubwa katika
biashara zao za kila siku.

No comments:

Post a Comment