IJUE HISTORIA YA NGUMI ZA KULIPWA UBINGWA WA AFRIKA MASHARIKI NA KATI (ECAPBF) ULIVYOANZA MWAKA 1983
LEO
tumeona ni vyema kuwakumbsha Watanzania na wapenzi wa ngumi kwa ujumja
ili kuweka kumbukumbu sahihi za taarifa kuhusu masuala ya ngumi za
kulipwa na ambazo tunafurahi kuwa zimeanza kutolewa na bwana Yasin
Abdallah (Ustaadh), tungependa pia kuwapa maelezo sahihi kuhusu ubingwa
wa Ngumi za Kulipwa wa Afrika ya Mashariki na Kati.
Ubingwa huu
umekuwa unapigiwa kelele na baadhi ya watu ambao wana malengo ya
kuharibu taswira nzima ya nguni za kulipwa na kuturudisha nyuma kwenye
enzi za vurugu zilizowahi kutokea hapo nyuma.
Ubingwa wa Ngumi za Kulipwa wa nchi za Afrika ya Mashariki na Kati ulianzishwa mwaka 1983 katika jiji la Nairobi nchini Kenya.
Mpaka kufikia
wakati huo (1983) ni nchi ya Tanzania pekee iliyokuwa imeshaanzisha
ngumi za kulipwa katika ardhi yake ambapo Kenya na Uganda zilikuwa bado
hazijaanzisha ngumi za kulipwa nchini mwao japokuwa zilikuwa na mabondia
kadhaa waliokuwa wanacheza ngumi za kulipwa katika nchi za Ulaya na
Asia.
Mabondia wa
Kenya waliokuwa wanacheza ngumi za kulipwa nje ya nchi yao wakati huo
walikuwa ni pamoja na Steven Muchoki na mdogo wake Michael Irungu,
waliokuwa wanapigana ngumi nchini Denmark chini ya Promota maarufu
Mogens Palle.
Mabondia wengine
wa Kenya waliokuwa wanapigana ngumi za kulipwa nje ya Kenya walikuwa ni
pamoja na Modesti Napunyi Oduor, Isayah Ikoni na Philip Warwinge
waliokuwa wanazipiga nchini Japan.
Aidha mabondia
wa Uganda waliokuwa wanacheza ngumi nje ya nchi yao waliongozwa na Ayub
Kalule, John Odhiambo, Mustapha Waisaja, John Mugabi (The Beast), John
Rubin Byaruhanga na Cuban Businge ambao wote pia walikuwa chini ya
promota maarufu Mogens Palle wa Denmark.
Kwa upande
Tanzania bondia pekee aliyekuwa anacheza ngumi za kukipwa nje ya nchi
wakati huo alikuwa Gerald Isaac (Tanzania’s Devil kama wapenzi wa ngumi
na vyombo vya habari vya Marekani walivyokuwa wanamwita kwa ajili ya
ukali wake kwenye masumbwi ulingoni) aliyekuwa anazichapa nchini
Marekani.
Tarehe 18
mwezi wa Juni liliandaliwa pambano la kwanza la aina yake kwa ubingwa
mpya kabisa wa Afrika ya Mashariki na Kati lililofanyika katika ukumbi
wa mikutano ya kimataifa jijini Nairobi (Kenyatta International
Conference Center, KICC).
Waandaji wa
mpambano huo walikuwa ni pamoja na DS Njoroge wa kampuni maarufu ya
ngumi wakati huo DS Boxing Promotions ya jijini Nairobi nchini Kenya,
Joe Akech ambaye wakati huo alikuwa ndiye Meneja Mkuu wa Kanda wa
shirika la ndege la Marekani, Pan American Airlines (Pan Am) na David
Attan na mkewe Linda Brown Attan wa kampuni ya Davlin Boxing Promotions
ambaye baadaye alikuja kuwa Promoter wa bondia Onesmo Ngowi.
Joe Akechi alikuja kuwa Mwenyekiti wa Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Kenya (KPBC) na Meya wa Jiji la Nairobi.
Mpambamno huo
wa kugombea mkanda wa Bantamweight uliwakutanisha mabondia wawili ambao
walikuwa wanatamba sana katika nchi zao katika miaka ya 1980!.
Bondia Onesmo
Alfred Ngowi (Piston Mover) wa Tanzania alikuwa ameshawapiga
mabondia wote waliokuwa tishio kwenye uzito wake wa bantamweight wakiwa
ni pamoja na Musa Mwabata, Sasi Sarungi, Ali Mohammed, Antoni Nyembela,
Pius Lwandalla na David Migeke.
Kwa upande
wa Kenya Modest Napunyi Oduor (Babaa) alikuwa ndiye bondia aliyekuwa
anatamba sana kwa wakati huo na ndio tu alikuwa anatokea nchini Japan
alikokuwa anapigana ngumi za kulipwa.
Wawili hao
(Ngowi na Oduor) walikutana katika mpambano wa kwanza kabisa wa Afrika
ya Mashariki na Kati tarehe 18 Juni 1983 katika ukumbi wa Kenyatta
International Conference Center (KICC) na kugombea mkanda wa kwanza wa
Afrika ya Mashariki na Kati.
Katika mpambano
huo mabondia wengine kutoka Kenya (Steven Muchoki, Athumani, na Michael
Irungu) Uganda (Cuban Businge) Tanzania (Clement Chacha, Emmanuel
Kimaro na Fidel Haynes) nao walipanda ulingoni kusindikiza pambano hilo
la kihistoria ambalo lilianzisha ngumi za kulipwa katika nchi za Kenya
na Uganda kwa mara ya kwanza.
Mwamuzi
wa mpambano huo wa ubingwa wa Afrika ya Mashariki na Kati alikuwa
Emmanuel Mlundwa wa Tanzania wakati huo akiwa ndiye Rais wa Boxing Union
of Tanzania (BUT) iliyokuja kubadili jina na kuwa Kamisheni ya Ngumi za
Kulipwa Tanzania (TPBC) mwaka 2000.
Miaka 21
baadaye mwaka yaani 2004, Kamisheni za Ngumi za Kulipwa za Kenya (Kenya
Professional Boxing Commission, UPBC), Uganda (Uganda Professional
Boxing Commission, UPBC na Tanzania Professional Boxing Commission, TPBC
zilikutana mjini Moshi na kuunda rasmi Shirikisho la Ngumi za Kulipwa
la Afrika Mashariki na Kati (East & Central Africa Professional
Boxing Federation au ECAPBF.
Katika mkutano
huo uliohudhuriwa na Marais wa Kamisheni hizo tatu Celestino Mindra
(UPBC) Memba Muriuki (KPBC) na Onesmo Ngowi (TPBC) uliweka uongozi mpya
wa Shirikisho la ECAPBF kama ifuatavyo:
Onesmo Ngowi (Tanzania) – Rais
Celestino Midra (Uganda) - Makamu wa Kwanza wa Rais
Memba Muriuki (Kenya) - Makamu wa Pili wa Rais
Shaaban Ogola (Kenya) Katibu Mkuu wa ECAPBF
Nemes Kaviehe (Tanzania) Mweka Hazina Mkuu wa ECAPBF
Paul Chiwa (Uganda) Afisa Uhusiano na habari Mkuu wa ECAPBF
Imetolewa na:
Uongozi
ECAPB
No comments:
Post a Comment