STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, July 23, 2014

HAWA NDIYO MASTA 10 WANAOVUTA MKWANJA MNENE DUNIANI



MTANDAO wa Forbes.com umetoa orodha ya  mastaa 10 wa kiume ambao wamelipwa pesa nyingi zaidi kwenye kazi zao za filamu. Muigizaji mweusi ni Will Smith peke yake kwenye Kumi Bora. Wasome hapo chini:
1 Robert Downey Jr – $75 million
2
2 Dwayne Johnson – $52 million
1
3 Bradley Cooper  – $46 million
3
4 Leonardo DiCaprio – $39 million
4
5 Chris Hemsworth – $37 million
6
6 Liam Neeson – $36 million
l
7 Ben Affleck – $35 million
5
8 Christian Bale – $35 million
chris
9 Will Smith – $32 million
dd
10 Mark Wahlberg – $32 million
dfff

HAWA NDIYO WASANII WAKALI ZAIDI BONGO

Kutoka kushoto, Irene Paul, Jacklyne Wolper na Riyama Ally
WAKATI Elizabeth Michael 'Lulu' akitajwa kama msanii wa kike wa filamu anayependwa na watu kupitia tuzo za 'Tanzania People's Choice Award', Jacklyne Wolper na Irene Paul wametajwa ndiyo wakali zaidi kati ya wasanii wa kike nchini.
Lulu alishinda tuzo mwezi uliopita sambamba na King Majuto na watangazaji wengine wa redio na runinga.
Hata hivyo katika utafiti uliofanywa na MICHARAZO kwa mwezi mmoja kwa kuhoji mashabiki wa filamu wasanii Wolper, Irene, Riyama Ally, Irene Uwoya, Shamsa Ford na Bi Hindu ndiyo  'walifunika' miongoni mwa waigizaji wa kike nchini.
Irene Paul, Shamsa na Wolper ndiyo waliotajwa mara nyingi na mashabiki wakifuatiwa na Riyama, Irene Uwoya, Bi Hindu, Mariam Ismail, Cathy, Sandra na Aunty Ezekiel.
Irene Paul ametajwa kama mmoja wa wasanii wa kike wenye kipaji halisi na wanaojua kugeukageuka katika nafasi yoyote na kusifiwa kupitia filamu za Fiona na 'Kibajaj'.
Uwoya yeye alipata kifyagio kupitia 'Ngumi ya Maria' na Apple wakati Wolper alifunika kupitia 'Ulimi' na 'Ndoa Yangu' aliyoigiza na marehemu Steven Kanumba.
Kwa upande wa waigizaji wa kiume waliotajwa kufunika ni  Jacob Stephen 'JB', Mohammed Mwikongi 'Frank', Kulwa Kikumba 'Dude', Nurdin Mohammed 'Chekibudi' na Amri Athuman 'King Majuto'.
Wengine katika 10 Bora ni Salum Mboto, Jimmy Master, Mtunisi, Gabo wa Zagamba na Mzee Jengua.

Yanga yampiga chini Kiiza, kisa Wabrazil

 
KLABU ya Yanga imembwaga mshambuliaji wake Mganda, Khamis Kiiza ‘Diego wa Kampala’ baada ya kusajiliwa kwa Wabrazil wawili, Andrey Coutinho na Geilson Santos Santana `Jaja`.Baada ya Jaja kusaini mkataba wa miaka miwili jana makao makuu ya klabu ya Yanga, kulikuwa na utata ni mchezaji gani atapigwa chini kati ya Kiiza na Emmanuel Anord Okwi.Awali ujio wa Jaja ulielezwa kuwaweka kitimoto Kiiza na Okwi, huku mmojawapo akitakiwa kutolewa kafara.
Taarifa za uhakika ambazo mtandao huu umezipata ni kwamba kocha Maximo amependekeza kuachwa kwa Kiiza kutokana na ripoti iliyoachwa na Hans Van Der Pluijm.
Mzigo huo uliofuatwa chini ya kapeti unasema kuwa Pluijm katika ripoti yake aliyowasilisha kwa viongozi baada ya kumalizika kwa msimu uliopita, alisema ili Emmanuel Okwi acheze Yanga sc, lazima Kiiza aondolewe.
Kwa kuzingatia mapendekezo hayo, Maximo amefuata ushauri huo na sasa Kiiza rasmi anaondoka Jangwani.
Katika hatua nyingine, imeelezwa na chanzo cha uhakika kuwa Maximo amewabana viongozi wa Yanga akiwataka wajenge uwanja wa mazoezi wa Kaunda ili kuepukana na adhaa anayoipata.
Maximo amewakazia na amesema hakuna jinsi, lazima uwanja huo ujengwe muda huu.
Pia amewataka viongozi kuboresha vyumba vya jengo la Jangwani ili wachezaji wote waishe pale.
Taarifa zinasema, Maximo amesema haiwezekani timu kukaa saa mbili kwenye foleni inapoelekea uwanjani na kurudi kambini.
Kwa mazingira hayo anataka wachezaji wake wakae makao makuu ya Yanga, mitaa ya Twiga na Jangwani, halafu uwanja wa Kaunda ujengwe.
Mbrazil, Marcio Maximo anafahamika kwa kuwa na msimamo mkali katika mambo yake.