STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, September 29, 2014

Vumbi Ligi Mabingwa Ulaya kutimka kesho

http://content.mcfc.co.uk/~/media/Images/Home/News/Team%20News/2014%2015%20season/Home%20Games/Chelsea%2021%20September/Group%20celebration%20close%20up.ashx?h=451&w=800
Manchester City watakuwa kubaruani kesho
https://pbs.twimg.com/media/Byc8SnZIcAAUeg-.jpg:large
http://e0.365dm.com/14/03/768x432/Bayern-Munich-celebrate_3101995.jpg?20140315195810
Bayern Munich kuendeleza ubabe wake Ulaya kesho?

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu ya England, Manchester City kesho inatarajiwa kutypa karata yake nyingine katika Ligi ya Mabingwa Ulaya wakati itakapowakaribisha As Roma ya Italia kwenye uwanja wa Etihad.
City itashuka nyumbani ikiwa na kumbukumbu ya kichapo cha bao 1-0 toka kwa Bayern Munich katika mechi yao ya raundi ya kwanza ya michuano hiyo.
Ikihanikizwa na ushindi wa ligi ya nyumbani City itahitaji ushinfi katika mechi ya kesho ya Kundi E ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kuwa miongoni mwa timu zitakazosonga mbele katika makundi.
Mbali na mechi hiyo inayotarajiwa kuwa na upinzani mkali kesho pia kutakuwa na michezo mingine kadhaa likiwamo pambano la CSKA Moscow ya Urusi itakayokuwa nyumbani kuvaana na Bayern Munich.
Katika mchezo wa kwanza CSKA ilichabangwa mabao 5-1 na Roma, hali inayofanya iwe na kazi ya ziada kama iliyonayo City katika kundi hilo.
Makundi mengine yatashuhudia timu za PSG watakuwa nyumbani kuikaribisha Barcelona katika mechi ya Kundi F, huku APOEL Nicosia ya Cyprus itawakaribisha Ajax ya Uholanzi.
Vinara wa EPL, Chelsea watakuwa ugenini mjini Lisbon kucheza na wenyeji wao Sporting Lisbon, katika mechi ya Kundi G ambalo pia litakuwa na pambano jingine kati ya NK Maribor ya Slovania itakayocheza na Schalke 04 ya Ujerumani.
BATE Borislov ya Belarus watawaialika Athletic Bilbao ya Hispania na Shakhtar Donetsk ya Ukraine wakiwa wenyeji wa FC Porto ya Ureno, hizo zikiwa mechi za kundi H.
Kipute kingine cha michuano hiyo kwa makundi yaliyobakia kitaendelea siku ya Jumatano.

Newz Alert! 200 wanusurika kifo Ruvuma kisa Togwa

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjO_S-l6Wfk0XGytRGNo_z8VxHh86vT54Eo2lXxFx74RVNuBVIyfcU3gfznTlm2molEPd2D4CDYNDyRg-K0THIp1m2ghBqMS87K9tPw0RwdyVvL5OoBAE9PxUnmBqQhJnlv6zBU7lnacT0/s640/DSCN1163.JPG
Picha haihusiani na habari hii, ingawa kinachoonekana pichani ni Togwa zikiwa sokoni

HABARI zilizotufika hivi punde zinasema zaidi ya watu 200 wamenusurika kufa baada ya kunywa Togwa linalosadikiwa kuwa na sumu katika kijiji cha Chitapwasi, mkoani Ruvuma.

Taarifa zaidi zitawajia kadri MICHARAZO itavayozipata kwa usahihi, ila inaelezwa baadhi ya walikumbwa na janga hilo wamekimbizwa katika vituo vya afya kwa ajili ya matibabu, japo haijafahamika kitu gani kilichosababisha watu hao kudhuriwa na togwa hilo, ingawa inahisiwa huenda ikawa na sumu.

Fainali Kombe la Shirikisho ni Al Ahly vs Sewe

http://www.en.beinsports.net/di/library/bein_sports/72/1d/ahly_3h4rvks5v5if1fs1rszi2ulm3.jpg?t=2095839318&w=670
Al Ahly ya Misri
http://en.starafrica.com/football/files/2013/04/615_340_SA_COTE-DIVOIRE_sewe-sport.jpg
Sewe Sports watakaokutana na Al Ahly kwenye fainali za Kombe la Shirikisho
BAADA ya kutemeshwa taji la Ligi ya Mabingwa Afrika, Al Ahly ya Misri imejiweka katika nafasi nzuri ya kujifariji kwa taji la Kombe la Shirikisho baada ya kufanikiwa kutinga Fainali ya michuano hiyo.
Timu hiyo iliyoing'oa Yanga kwenye mechi ya raundi ya pili ya Ligi ya Mabingwa mapema mwaka huu, imetinga hatua hiyo baada ya kuifunga Coton Sports ya Cameroon kwa mabao 2-1 katika nusu fainali.
Katika mechi ya kwanza Al Ahly walishinda ugenini bao 1-0 na ushindi huo wa jana umewafanya kufuzu Fainali kwa jumla ya mabao 3-1.
Kwa maana hiyo wababe hao wa Afrika watavaana na Sewe Sports ya Ivory Coast iliyotangulia mapema kwa kuinyoa AC Leopards ya Congo.
Mechi za hatua hiyo zitachezwa mwishoni mwa Novemba na mwanzoni mwa Desemba na kujulikana bingwa mpya wa michuano hiyo baada ya taji kuwa wazi lililokuwa likishikiliwa na Sfaxien ya Tunisia walioshiriki Ligi ya Mabingwa na kutolewa na AS Vita.

Rais JK kuzindua barabara ya Mwenge-Tegeta

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhMk0vSfAt8jHtAhakSB7WvHhsiQsyDQ3FoVsGoT4CpB8NFGVSWDMGy9-1pUHS72qegQZeRSFWebW5m5lv_B4-EU6g2bcOeMM9YVnPkQzhIBcv7Ic0C6xVbuGr8psoDH6RoLFLzsQQfcdGw/s640/Rais+Jakaya+Kikwete+%2528kati%2529+Balozi+wa+Japan+nchini+Hiroshi+Kanagawa+%2528kulia%2529+wakikata+utepe+na+Waziri+wa+Ujenzi+John+Mgufuli+aki.jpg
Rais Kikwete alipozundua ujenzi wa barabara hiyo

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhp1HUk3XqXz8wzRf9snLC3eY5TZp0maO9SMNksDsdurpQID42Ap96Wk5H78DmTjJq-GN6GxnPmCH6i3CQOTvsD6jNZ-P3oe-NWWnqretJxzG4GNmtGesW7yB8TP4w2iT_QRaUDPyfH_Cc/s1600/20140511_123729.jpg
Barabara ya Mwenge Tegeta

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika sherehe za ufunguzi wa barabara ya Mwenge –Tegeta yenye urefu wa kilometa 12.9 katika eneo la Lugalo, jijini Dar es salaam.  

Taarifa iliyotolewa leo jijini Dar es salaa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Muhandisi  Musa Iyombe imeeleza kuwa sherehe za ufunguzi wa barabara hiyo zitafanyika tarehe 1, Oktoba ,2014 katika eneo la Lugalo njia panda ya Kawe kuanzia saa nne asubuhi.
Taarifa  hiyo imeeleza kuwa kukamilika kwa upanuzi wa barabara hiyo yenye urefu wa kilometa 12.9 ni sehemu ya mkakati wa serikali wa kupunguza msongamano wa magari katika jiji la Dar es salaam.
Aron Msigwa –MAELEZO.
29/9/2014.
MWISHO.

TID 'Mnyama' kufyatua na Tumi Molakane

MNYAMA TID, yupo hatua ya mwisho kukamilisha 'ngoma' yake mpya inayoenda kwa jina la 'Bongo' aliyomshrikisha rapa kutoka Afrika Kusini aiywao Tumi Molakane.
Kazi hiyo ya kwanza kwa TID kufanya na msanii huyo maarufu nchini mwake, imerekodiwa katika studio za B Records.
TID alidokeza kuwa kwa kitambo kirefu alikuwa akimwinda rapa huyo na kufanya naye mawasiliano kupitia mitandao ya kompyuta kabla ya kumzukia Dar na kuingia naye studio kufanya wimbo huo.
Staa huyo wa 'Zeze', 'Girlfriend', 'Nyota' na 'Voice of Prison' aliwataka mashabiki wake wajiandae kusikia 'kolabo' hiyo wakati akifanya mchakato wa kwenda Afrika Kusini baadaye ili kutengeneza video yake.
"ViDeo ifanywa Afrika Kusini ili kuleta ladha kulingana na ushiriki wa Tumi," alisema TID..

Tanzia! Side Boy Mnyamwezi Hatunaye

HABARI zilizotufikia hivi punde zinasema kuwa aliyekuwa msanii wa Bongo Fleva aliyewahi kutamba na nyimbo za 'Kua uone', 'Usimdharau Usiyemjua' na Hujafa Hujaumbikam, Side Boy Mnyamwezi amefariki.
Kwa mujibu wa taarifa za mdogo wake Ally Khamis, Side Boy ambaye majina yake kamili ni Said Salum Hemed amefariki nyumbani kwao Lindi.
Taarifa zinasema kuwa marehemu kabla ya mauti yaliyomkuta katika Hospitali ya Mkoa wa Lindi ya Nyangao alikuwa akisubumbuliwa na maradhi ya TB.
MICHARAZO inawapa pole wote walioguswa na msiba huu, hasa ikizingatiwa iliwahi kuandika makala yake ndefu ya kisanii na mipango yake.
Mungu Ailaze Roho ya Marehemu Mahali Pema Peponi.

Sunday, September 28, 2014

Kavumbagu hashikiki, Ruvu Shooting 'kavukavu'


http://hivisasa.co.tz/wp-content/uploads/2014/09/DSC04592.jpg
Kavumbagu (kushoto) akishangilia moja ya mabao yake na wachezaji wenzake wa Azam
WAKATI Didier Kavumbagu akiendelea kuongoza kwenye orodha ya wafungaji wa mabao mpaka sasa ligi ikiwa imemaliza mechi za raundi ya pili, Ruvu Shooting inayonolewa na kocha Tom Oloba ndiyo timu pekee ambayo haijaambulia pointi hata moja mpaka sasa.
Pia Ruvu ni kati ya timu mbili ambazo hazijatikisa wavu wa timu pinzania katika ligi hiyo ikienda sambamba na ndigu zao wa JKT Ruvu ambayo leo imefumuliwa mabao 2-0 na Kagera Sugar jijini Dar es Salaam.
Azam wamekalia kiti cha uongozi wa ligi hiyo licha ya kulingana kila kitu na Mtibwa Sugar kutokana na kubebwa na herufi A.
Ndanda waliokuwa wakiongoza msimamo huo baada ya mechi za ufunguzi, imeporomoka hadi katika nafasi ya nne ikipitwa na Mbeya City wanaokamata nafasi ya tatu.
Didier ndiye kinara wa mabao mpaka sasa akiwa na mabao manne, hali inayoashiria kwamba Yanga walifanya kosa kubwa kumuacha mchezaji huyo kutoka Burundi aondoke Jangwani ilihali kwa misimu miwili mfululizo akiwa na kikosi hicho alikuwa kinara wa mabao ya Yanga.
Hata hivyo ni mapema kutabiri kama Kavumbagu atatimiza ndoto za kutwaa kiatu cha Dhahabu alichokikiosa kizembe msimu wa 2012-2013 baada ya kuzidiwa na Kipre Tchetche licha ya kumaliza duru la kwanza la msimu huo akiongoza orodha ya wafungaji.
Didier anafuatiwa na Ame Ally na Shomary Ally wa Mtibwa wenye mabao mawili kila moja huku orodha ya wachezaji wenye bao moja moja ikiongozwa na nyota wa Simba na Yanga, Emmanuel Okwi na Coutinho walianza kufunga mabao katika mechi zao za wikiendi hii dhidi ya timu za Polisi Moro na Prisons.


MSIMAMO LIGI KUU TANZANIA BARA 2014-2015
                                                P  W  D  L  F  A  Pts
1. Azam                                   2   2   0   0  5   1   6
2. Mtibwa Sugar                     2   2   0   0  5   1   6
3. Mbeya City                        2   1   1    0  1   0   4
4. Ndanda Fc                          2   1    0   1  5   4   3
5. Prisons                                2   1    0   1  3   2   3
6.Kagera Sugar                      2    1   0   1  2   1   3
7.Yanga                                   2    1    0  1  2   2   3
8. Mgambo JKT                     2    1   0   1  1    1  3
9.Stand Utd                             2    1   0   1   2   4  3
10.Simba                                 2    0   2   0   3   3  2
11.Coastal Union                    2    0   1   1   2   3  1
12. Polisi Moro                       2    0   1    1  2   4  1
13.JKT Ruvu                          2    0   1    1  0   2  1
14. Ruvu Shooting                  2    0   0    2  0   4  0

TCAA yatumia Sh. Mil 490 kusomesha marubani wa5

http://www.fullshangweblog.com/wp-content/uploads/2013/08/IMG-1.jpg
Bestina Magutu (kushoto)
Na Kipimo Abdallah
MAMLAKA ya Usafiri wa Anga Tanzania TCAA imetumia dola 310,000 sawa na shilingi milioni 496 kwa ajili ya kuwalipia ada wanafunzi watano ambao wanasomea urubani wa ndege nchini Afrika Kusini.
Hayo yamebainishwa na Afisa habari wa TCAA  Bestina Magutu wakati akizungumza na mwandishi wa habari hii jijini Dar es Salaam.
Alisema wanafunzi hao wamepatikana baada ya mchujo wa wanafunzi 270 ambao waliomba ambapo walibakia 11 na baadae ndio  wakapatikana hao awatano ambao wanalipiwa na TCAA.
Magutu alisema ufadhili ni kwa kila mwanafunzi kupatiwa dola 62,000 ambazo ni zaidi ya shilingi milioni 99 za Kitanzania ambapo watasoma kwa miezi 14 na mwishoni mwa mwa huu watakuwa wanahitimu.
Alisema jitihada za TCAA ni kuhakikisha kuwa idadi ya marubani inaongezeka kila mwaka ukizingatia kuwa wapo ambao wanastaafu na wengine wakifariki hivyo bu wajibu wa mamlaka hiyo kuongeza watu wa tasnia hiyo.
“TCAA tunajitahidi kuwapatia ufadhili wanafunzi ambao wanakuwa na sifa za kusoma urubani ambapo kwa sasa wapo watano wako Afrika Kusini ila gaharama ni kubwa hivyo tunaomba wadau kujitokeza kufanikisha zoezi hilo”, alisema Magutu.
Afisa Habari huyo wa TCAA alisema hadi kufikia mwezi Julai mwaka huu idadi yamarubani ilikuwa 562 idadi ambayo ni ndogo kutokana na ukweli kuwa kumekuwepo kwa ongezeko kubwa la uwekezaji katika sekta hiyo.
Magutu alisema iwapo Serikali itaachiwa yenyewe katika kutoa mafunzo ya urubani ni wazi kuwa idadi itakuwa ndogo hali ambayo itachangia kazi nyingi kuchukuliwa na watu kutoka nje.
Alitoa wito kwa jamii kushirikiana ili kuhakikisha kuwa nchi inakuwa na idadi kubwa ya watu wenye fani ya urubani ili kuhakikisha kuwa fursa zinazojitokeza wanaziitumia ipasavyo.
Aidha akizungumzia ni kwa nini wanafunzi hao wanaenda kusoma nje ya nchi na sio hapa nchini Ispecta Mwandamizi wa Idara ya Udhibiti Masuala ya Usalama wa Ndege Redemptus Bugomola alisema vyuo vilivyopo hapa nchini vinatoa elimu ya urushaji ndege za watu binafsi jambo ambalo haliwezi kukidhi hitaji la ndege za kibiashara na zile kubwa.
Bugomole alisema sekta anga ni moja ya sekta ambayo inahitaji uwepo wa watu wenye nia madhubuti ya kusoma kutokana na ukweli kuwa matumizi yake yanhitaji umakini wa hali ya juu.

Pambano la Nasibu na Matumla Jr hakuna mbabe

Bondia Mohamed Matumla kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Nasibu Ramadhani wakati wa mpambano wao uliofanyika jana katika ukumbi wa Friends Corne Manzese Dar es salaam mpambano huo ulitoka droo za kufungana pointi.
Bondia Mohamed Matumla kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Nasibu Ramadhani wakati wa mpambano wao uliofanyika jumamosi katika ukumbi wa Friends Corne Manzese Dar es salaam mpambano huo ulitoka droo za kufungana pointi
Bondia Lulu Kayage akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Fatuma Yazidu wakati wa mpambano wao Yazidu alishinda kwa pointi mpambano huo.
Mabondia wa kike Fatuma Yazidu kushoto na Lulu Kayage wakioneshana umwamba wa kutupiana makonde wakati wa mpambano wao uliofanyika jumamosi katika ukumbi wa Friends Corne Manzese Dar es salaam Yazidu alishinda kwa point mpambano huo.
Mabondia wa kike Fatuma Yazidu kushoto na Lulu Kayage wakioneshana umwamba wa kutupiana makonde wakati wa mpambano wao uliofanyika jumamosi katika ukumbi wa Friends Corne Manzese Dar es salaam Yazidu alishinda kwa pointi.
Mabondia wa kike Fatuma Yazidu kushoto na Lulu Kayage wakioneshana umwamba wa kutupiana makonde wakati wa mpambano wao uliofanyika jumamosi katika ukumbi wa Friends Corne Manzese Dar es salaam Yazidu alishinda kwa point mpambano huo.
Bondia Lulu Kayage akilalamikia matokeo ya kupigwa na Fatuma Yazidu kulia ni bondia Ibrahimi Class 'King Class Mawe'
Mabondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe'  kushoto na Shomari Milundi wakifuatilia mpambano huo pamoja na mashabiki mbalimbali
Mabondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe'  kushoto na Shomari Milundi wakifuatilia mpambano huo
 
Mabondia Juma Bigilee kushoto,Ibrahimu Class ; King Class Mawe' na Rashidi Mhamila wakiwa katika pozi baada ya mchezo kumalizika

Kingunge awashushua wanaoiota Tanganyika


https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg1ZYzBGLwXu0x9UUT0731EMnVXnS3ORTl2ardjjCveW-DptFDEfVH4KiZtdRSjy-RZaWJ6k-0A3U6UVSj9aE2xoIG-Si79w_J4GMZifJDM8J2GG4KTLYy16Jly2XJvEc7vHbKbLanG6w59/s1600/DSCF0347.JPG 
Na Kipimo AbdallahWAKATI suala la Utanganyika na Utanzania liendelea kukuna vichwa vya wanasiasa na wananchi wa kada mbalimbali Mwanasiasa Mkongwe Mzee Kingunge Ngombale Mwiru amewataka watanzania wasahau hilo na kujitambua kuwa wao ni Watanzania.
Kauli hiyo ya Ngombale Mwiru inakuja ikiwa ni muda mchache baada ya Mjumbe mwenzake ambaye pia ni Mbunge wa Bunge la  Maalumu la Katiba John Cheyo kusema itakuwa ngumu kwa jamii kuondolewa dhana ya kuwaTanganyika haipo.
Mzee Ngombale Mwiru alisema ni jambo la kusikitisha kuona watu wanaitaja Tanganyika wakati wakijua kuwa hiyo ni historia ya aibu kwa Watanzania ambao walikuwepo katika kipindi hicho cha ukombozi wa Taifa hili.
Ngombale Mwiru alisema jambo la kushangaza wapo watu ambao hata Tanganyika hawajaishuhudia lakini wameonekana kuwa na nguvu ya kuhitaji uwepo wake jambo ambalo linapotosha jamii.
“Kwa kweli sikuwa na dhamira ya kulizungumzia suala hili ila nimeshawishika baada ya kuona mzee mwenzangu kuongea na kuonyesha kuhitaji Tanganyika jambo ambalo mimi nalipinga kwa nguvu zote kwa sababu najua historia yake haina maana kwa Watanzania wa leo” alisema.
Aidha Mzee Ngombale Mwiru alitoa wito kwa jamii kusoma historia ya nchi hii ili kuhakikisha kuwa wanapata takwimu sahihi za nchi yao ili kuacha tabia ya kufuata mkumbo ambao hauna tija kwa maslahi ya Taifa.
Akichangia katika Bunge hilo Mbunge wa Bariadi Mashariki John Cheyo alisema itakuwa ngumu kuisahau Tanganyika kutokana na ukweli kuwa ndiyo msingi wa uwepo wa Tanzania.
Cheyo alisema haiwezekani Zanzibar ikaendelea kuwepo na kutambulika na Tanganyika ikasahaulika katika mazingira ya kawaida kama baadhi ya viongozi wengine wanavyotaka.
Mjumbe huyo wa Bunge la Katiba alisema ni vema jamii ikapatiwa elimu ya kutosha ili kuhakikisha kuwa ufahamu unakuwepo wa kutosha ili kila Mtanzania aweze kuwa na uelewa juu ya nchi yao.
 Kwa upande mwingine Cheyo amewataka wabunge kutoka Zanzibar wasije kuzuia haki za Watanzania Bara wanaozidi milioni 47 wakati wa upigaji kura ili kuhakikisha kuwa Katiba hiyo inayopendekezwa inapita.
Cheyo alisema idadi ya wazanzibari ni ndogo ila ina nguvu katika mchakato mzima wa kupatikana kwa katiba ambayo itaweza kulinda muungano wa nchi au kuuvunja.
Alisema lipo suala la aina ya muungano ambalo limeweza kuleta malumbano makubwa sana katika Bunge hilo hivyo ni vema suala hilo likatafakariwa vizuri ili kuhakikisha kuwa kila upande unaridhika kwa maslahi ya Taifa.
Cheyo alisema itakuwa vizuri iwapo fursa itapatikana kwa wahusika kutoa nafasi kwa wananchi kupiga kura dhidi ya aina gani ya muungano wanaoutaka ili kuhakikisha kuwa suala hilo limetatuliwa.
Mbunge huyo wa Bunge la Katiba alitoa rai kwa baadhi ya wanasiasa na wanaharakati ambao wanaendelea na harakati za kuhamasisha jamii kupinga Bunge hilo waachane na mpango huo kwani wao wapo kihalali.
Alisema Kituo Cha Demokrasia (TCD) kipo hivyo wanapaswa kukitumia ili kuhakikisha kuwa wanafikia muafaka kwa maslahi ya Taifa na sio kung’amg’ania maandamano ambayo yanahatarisha maisha ya watanzania.

Kapteni Ligora awapasha wanasiasa wanaolumbana

http://3.bp.blogspot.com/-eqAX732KQAk/U_CoM9ap3ZI/AAAAAAAAWP4/wTE9EfEZszs/s1600/WAZEE%2B01.jpg
Na Kipimo AbdallahKATIBU Mkuu Mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Dar es Salaam Kapteni Mstaafu Mohammed Ligora amewataka wanasiasa kuacha kulumbana juu aina ya katiba kwani wenye maamuzi ya mwisho ni wananchi ambao watapiga kura.
Ligora alisema hayo jana ikiwa ni siku chache baada ya kuonekana hali ya sintofamu juu ya hatma ya katiba pendekezwa ambayo imesomwa na Mweyekiti wa Kamati ya Uandishi Adrew Chenge.
Alisema anapatwa na mshangao dhidi ya baadhi ya viongozi ambao wamekuwa wakiendeleza malumbano kupitia vyombo vya habari huku wakitambua kuwa wenye maamuzi ya mwisho dhidi ya aina ya serikali na mambo mengine ni wananchi.
Kapteni Mstaafu huyo alisema ni vema viongozi wa kisiasa pamoja na wale wanaoitwa watetezi wa haki za wananchi kujikita katika harakati za kujenga nchi hasa pale ambapo inaonekana kuwa Chama Tawala na Serikali yake kimeshindwa kufanya vizuri.
“Napenda kutoa rai kwa wanasiasa na wanaharakati kujitikita katika masuala mengine yenye tija kwa nchi kwani hili la katiba muafaka wake upo chini ya wananchi wenyewe ambao ndio wataamua kuwa katiba iwepo au la”, alisema Ligora.
Katibu Mstaafu huyo alisema jamii ya Kitanzania ina watu wengi ambao wameelimika hivyo hawahitaji kufanyiwa maamuzi ambayo yanaweza kuwa na maslahi kwa watu wengine ambao wanajiita wanasiasa.
Aliwataka wananchi kufanya maamuzi ambayo yatakuwa yamezungukwa na utashi wao bila kushurutishwa na mtu yoyote kwani nchi ya Tanzania ni ya kila mtanzania bila kuangalia rangi, elimu na ukabila.
Kwa upande mwingine Kapteni Mstaafu huyo alisema ni wakati wa vyama vya siasa kuonyesha ushirikiano mkubwa ili kuweza kudumisha umoja, amani na utulivu wa Taifa la Tanzania ambalo limejaliwa jamii yenye upendo.
Alisema kasoro ambazo zimeonekana katika mchakato mzima wa kutengeneza katiba zisiwe sababu ya kupelekea Taifa katika machafuko kwani madhara yake yatakuwa ya muda mrefu kwa jamii ya Watanzania.
“Unajua suala la kujitambua ni muhimu katika maamuzi ili kuhakikisha kuwa maamuzi yote tunayofanya yanakuwa na weledi jambo ambalo mimi naamini asilimia 80 ya watanzania inajitambua”, alisema.

Yanga yaizima Prisons, Coutinho atupia, Kagera yaiua JKT Ruvu

http://api.ning.com/files/TQDVHBx0tuW3uYd3Hlc1u9fa7CEF04w*k4I94R9HrkYatgIrq-g2atl0ZzYAt9xFoxdmCIGWif22TfQkM6XSLf9MqO1vd*6b/COUTINHO.jpg
Coutinho aliyerejea na bahati jangwani
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh_4EFuv2AZMTxTK507IEk38peIzLAvmxPWIcSIvLbGm663MNQQM752-EFBTwep6sws02MX1e0tsQRe-9Bs8XPyf_EXN47h0kQW7lAgkPsiZ2GecmjTGDD69kMxpjOPUXh57GikV7gUB081/s1600/Yanga+iliyobeba+Ngao+ya+Jamii.JPG
Yanga
Prisons-Mbeya
KIUNGO mshambuliaji Andrey Coutinho amerejea dimbani na mguu wa Bahati baada ya kuisaidia Yanga kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Prisons-Mbeya katika mfululizo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Coutinho aliyekuwa majeruhi aliifungia Yanga bao dakika ya 34 kwa mkwaju wa adhabu baada ya Mrisho Ngassa aliyesumbua katika mechi ya leo kuangushwa mita 25 toka lango la Prisons.
Bao hilo lilidumu hadi wakati wa mapumziko licha ya Yanga kukosa mabao mengi ya wazi kupitia kwa Genilson Santana 'Jaja' huku Prisons wakiwa pungufu baada ya mchezaji wao mmoja kuonyeshwa kadi ya pili ya njano na mwamuzi Andrew Shamba dakika chache baada ya bao la Yanga kwa kumchezea vibaya Ngassa.
Kipindi cha Prisons waliingia wakiwa tofauti na kuliandama lango la Yanga na kufanikiwa kusawazisha bao dakika ya 64 kupitia kwa Ibrahim Kihaka, ingawa Yanga ilijibu mapigo dakika mbili baadaye kupitia kwa Simon Msuva aliyefunga bao la pili lililoisaidia kuipa Yanga pointi tatu za kwanza na kuchupa toka mkiani hadi katika nafasi za kati ikiwa na pointi nne.
Katika mechi nyingine ya pili hiyo iliyochezwa uwanja wa Chamazi, maafande wa JKT Ruvu wameshindwa kuhimili vishindo vya wakata miwa wa Kagera Sugar baada ya kukubali kipigo cha amabo 2-0.
Mabao ya washindi yalifungwa kila kipindi na wachezaji Salum Kanoni na Rashid Mandawa na kuifanya kagera kufikisha pointi tatu baada ya mechi mbili tangu kuanza kwa ligi hiyo wiki iliyopita.

TP Mazembe yashinda, ila yakwamba kucheza Fainali Afrika

tpess22
Voir l'image sur Twitter
Kipa wa Mazembe akilia huku akitulizwa na mchezaji wa ES Setif
Voir l'image sur Twitter
Ilikuwa vita
LICHA ya kupata ushindi wa mabao 3-2 nyumbani mjini Lubumbashi, TP Mazembe imeshindwa kuwapa fursa nyota wa Kitanzania, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu kucheza kwa mara ya kwanza Fainali za Ligi ya Mabingwa Afrika.
Mazembe ilimejikuta waking'oka kwenye hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo baada ya matokeo ya mwisho kuwa mabao 4-4 baada ya awali kufungwa ugenini na ES Setif ya Algeria kwa mabao 2-1.
Katika mechi iliyomalizika jioni hii, Mazembe ilihitaji ushindi wa aina yoyote usio wa magoli, kitu ambacho hata hivyo hakikutokea baada ya kuruhusu wageni kupata mabao yaliyowabeba kutinga Fainali.
Wageni waliwaduwaza Mazembe kwa kuandika bao dakika ya 9 tu ya mchezo kupitia Ziaya kabla ya Adjei Nii kusawazisha kwenye dakika ya 21 na kufanya matokeo kuwa bao 1-1.
Coulibaly aliiongezea Mazembe bao katika dakika ya 38 na kufanya waende mapumziko wakiwa nguvu sawa ya jumla ya mabao 3-3 ukijumlisha na mechi yao ya awali.
Mbwana Samatta alimtengenezea Bolingui pande safi na kuandika bao la tatu dakika ya 53 na kuonekana kama Mazembe wanaelekea kufuzu fainali hizo za Afrika.
Hata hivyo Younès kuifungia Setif bao muhimu dakika ya 75 na kufanya hadi mwisho matokeo kuwa mabao 3-2 Mazembe wakishinda, lakini waking'oka na kuwakosesha akina Samatta kuweka rekodi ya kuwa Watanzania wa Kwanza kucheza fainali za Afrika.
ES Setif sasa itapambana na AS Vita pia ya DR Congo ambayo jana iliweka rekodi baada ya kuwang'oa Sfaxien ya Tunisia kwa jumla ya mabao 4-2 kufuatia ushindi wa kushangaza wa mabao 2-1 ugenini.
Katika mchezo wa kwanza wiki iliyopita Vita ilishinda pia mabao 2-1.

Saturday, September 27, 2014

Pascal Ndomba ampania Francis Cheka Morogoro

http://www.thisday.co.tz/media/picture/large/Boxing.jpg
Pascal Ndomba
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjw8LmdtQarvRbtu2no4R1hcuEdxu1zGNK2lAmGpagaOyI3Bem_cLLA8XVo2JKPzaMdMNNrg2OsGmQMtC2kmvwmYr1HmUYcu_syCvVzxmyX3BqGqcSwGzWebz-wvcCmNPi2kU9q7-oNcQ5y/s1600/Bondia-Francis-Cheka.jpg
Francis Cheka
 BONDIA Pascal Ndomba anayetarajiwa kupanda ulingoni Novemba Mosi kupigana na aliyekuwa Bingwa wa Dunia wa WBF, Francis Cheka wiki ijayo anatarajiwa kuingia kambini kujiwinda na pambano lisilo la ubingwa.
Aidha bondia huyo ametamba kumsambaratisha Cheka ili kuvunja mwiko wa kutopigwa na bondia yeyote katika ardhi ya Tanzania tangu mwaka 2008.
Mabondia hao watapambana kwenye uwanja wa Sabasaba mjini Morogoro katika uzito wa Light Heavy raundi 8.
Akizungumza na MICHARAZO, Ndomba alisema ataingia kambini wiki ijayo kujiandaa na pambano hilo akiwa na nia moja tu ya kumtandika Cheka na kuziba ubabe kwa mabondia wa Tanzania.

Nahodha Coastal Union awaponda akina Jaja

NAHODHA wa timu ya Coastal Union, Mbwana Kibacha amewaponda washambuliaji wa kulipwa wa klabu za Simba na Yanga akiwamo Genilson Santana 'Jaja' akidai hawa lolote zaidi ya kubebwa na vyombo vya habari.
Kibacha alisema viwango vya Jaja na wengine wanaoichezea Yanga na wale wa Simba ni wa kawaida mno tofauti na waliopo Azam aliowafagilia akidai ni moto wa kuotea mbali.
Akizungumza katika mahojiano maalum na MICHARAZO, Kibacha aliyepewa mikoba ya unahodha baada ya kuwa msaidizi wa Juma Nyosso msimu uliopita ambaye kwa hayupo kikosini humo..
"Mapro wa Simba na Yanga ni wa kawaida sana, hawana viwango vya kutisha ila wanafagiliwa na kupambwa sana na magazeti kiasi cha kuwafanya waonekane kama akina Cristiano Ronaldo au Angel di Maria.
Beki huyo alikiri kuwa, wachezaji wanaostahili kuendelea kuwepo nchini kwa viwango vyoa vya soka ni wale waliopo Azam na pengine wenzake anaocheza nao Coastal Union.
"Mapro wa Azam ni wa ukweli, lakini waliopo Simba na Yanga wanapambwa tu kwenye magazeti, hawana lolote, wanazidiwa hata na wakali wetu wa Coastal Union," alisema Kibacha.

Washindi TMT warekodi filamu ya aina yake 'TMT Movie'

https://thumbp22-ne1.mail.yahoo.com/tn?sid=2126005954&mid=AKh2imIAABCBVCU0VAAAAE%2FiWx0&midoffset=2_0_0_1_3332247&partid=7&f=1214&fid=Inbox&m=ThumbnailService&w=3000&h=3000
Baadhji ya washiriki wa filamu hiyo ya TMT Movie
WASHINDI wa shindano la kusaka vipaji vya filamu nchini, TMT, wakishirikiana na wakali wengine wa fani hiyo wanatarajiwa kuibuka na filamu ya aina yake iitwayo 'TMT Movie' ambayo imewashirikisha wasanii zaidi ya 200.
Kwa mujibu wa mratibu wa filamu hiyo, Staford Kihore, filamu hiyo imeanza kurekodiwa ikiwa ni moja ya malengo ya Proin Promotion iliyoendesha shindano la TMT, kuwajenga wasanii wa filamu na kuwapa uwezo wa kuigiza na kufanya kazi kimataifa.
Kihore alisema kuwa wanataka kuthibitishia umma kwamba TMT haikuwa kazi bure bali kuwafanya wenye vipaji vya fani hiyo 'kutusua' ili wafike mbali ndani na nje ya nchi.
“Tasnia ipo na inafanya vizuri lakini inahitaji uthubutu kwa kati ya wanaotengeneza sinema wawe tayari kufanya kitu kizuri kinachoweza kuvuka mipaka ndio tunachokifanya sasa baada ya kuwatengeneza kitaaluma wanafanya kazi,”anasema Staford.
Wasanii wa TMT wamefundishwa na kuiva katika fani ya uigizaji na moja ya alama yao wanayojivunia ni pale ambapo wamepewa nafasi ya kuonyesha uwezo wao kupitia filamu ya TMT Movie na kuonyesha kile wanachoongea kwa watazamaji na wapenzi wa filamu Swahilihood.
Filamu kubwa ya TMT Movie inatarajiwa kuonyeshwa katika majumba ya Sinema Afrika Mashariki na Ulaya pia sinema inaongozwa na Muongozaji mahiri wa filamu Karabani na imeandikwa na Novatus Mgulusi ‘Ras Nova’ zaidi ya wasanii 200 kushiriki katika filamu hiyo.
Mhusika mkuu wa filamu hiyo ni Milionea kutoka Mtwara kwa maana mshindi wa shindano la TMT, Mwanaafa Mwizango na nyota wote wa TMT, huku wasanii nyota kibao kutoka tasnia ya filamu Bongo wakipatia nafasi za ushiriki wa filamu hiyo inayojenga ajira kwa jamii nzima.

TCAA yatumia Mil. 200 kuboresha ya Mawasiliano Mnyusi Tanga

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjgp92-UaJEj1Q0BjT_TDJlnGpzbAF6zP5KT-cZH_G44BNiUmbX0m6g_APf_eQrmnpcrKGydWuifPpvWnpx42jPfxzImYnUADbpageNtG_fXTkJGadqNeUsvun0rVvuBDXPKuHc4fzxRf0/s1600/1.jpgNa Kipimo Abdallah
ZAIDI ya shilingi milioni 200 zimetumika katika maboresho ya kituo cha mawasiliano cha Mnyusi mkoani Tanga kinachotumika kupokea na kutuma mawasiliano ya radio zinazo tumika katika usafiri wa anga.
Hayo yamebainishwa na Afisa habari wa TCAA  Bestina Magutu wakati akizungumza na mwandishi wahabari hii leo jijini Dar es Salaam.
Alisema maboresho hayo yametokana na ukweli kuwa kituo hicho kilikuwa hakifanyi kazi kwa muda mrefu hali ambayo ilikuwa inaasababisha kukosekana kwa mawasiliano katika ukanda wa mashariki kutoka usawa wa bahari.
Kabla ya kukamilika kwa maboresho haya baadhi ya maeneo mchini yalikuwa hayapati mawasiliano ya kitekonologia kutoka nchini na badala yake walikuwa wanapata huduma hiyo kutoka nchi jirani,"alisema.
"Mradi huo umekamilika na kukabithiwa kwenye mamlaka ya usafiri wa anga mwezi agost mwaka huu na kukabithiwa kwenye kituo cha Mnyusi jijini Tanga,umegharimu shilingi za kitanzania milioni 292,887,921," alisma.
Magutu aliongeza kuwa kukamilika kwa mradi huo kumeongeza ufanisi wa usafirishaji wa anga kwa kurahisisha huduma ya kuongoza ndege,utaongeza mapato kwa mamlaka hiyo.
"Nimategemeo yangu kwamba kupitia maboresho haya mamlaka itajiongezea mapato kupitia tozo ya huduma ya uongozaji ndege,
Kwa upande wake Mkaguzi Mwandamizi,Redemptus Rugombe alisema mamlaka inandelea kupanua miondombinu ya kuongeza ndege sanjari na mabadiliko ya teknolojia ili kumudu ukuaji wa sekta ya usafirirshaji wa anga.
"Takwimu za mwaka 2031 zinaonyesha ongezeko la miruko ya ndege (flight movement) imeongezeka hadi kufikia miruko 230,458 sawa na ongezeko la asilimia3.6 kotoka miruko 222,430 mwaka 2012,
Kadharika katika kipindi hicho idadi ya abilia imeongezeka kutoka 4,056,925 hadi kufikia 4,626,016 sawa na ongezekola asilimia 14,kwa sasa idadi ya abilia inatarajiwa kuongezeka zaidi kufikia mwishoni mwa mwaka huu," alifafanua.
Mkaguzi Mwandamizi huyo aliongeza kuwa katika kuhakikisha watanzania wanapata uelewa wa elimu ya mamlaka ya anga mamlaka inaendelea kuwapatia wanafunzi mafunzo kwa njia ya udhamini na hadi sasa kuna wamnafunzi watano wanaendelea ma mafunzo ya urubani.
"Kwa tarifa za wanafunzi wetu ambao wako Afrika ya kusini kwa masomo ya urubani chini ya udhamini wa mamlaka wanaendelea vizuri,huu mpango kwa mamlaka ni endelevu ili kusaidia kuwawezesha watanzania kpambana katika soko la ajira, "alisema.

'Ukosefu wa Uwazi ni Chanzo cha Rushwa Tanzania'

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjkqiPQsLR4dR34JMnoJdhbpwxbdoCH-qTpWAryh64hEFJ3U23QoYIqWJRVJzCBmxplRC27H-FamXQELVjYYcJegteGyTz0EcgBPUe0yRr9IqH-fe3UT5ZbVs7VxW8zMK9kw-EnhUbvf9I/s640/dkhosea.jpg
Mkurugenzi wa TAKUKURU, Dk  Hosea

Na Kipimo Abdallah
KUTOKUWEPO kwa uwazi, uadilifu na uwajibikaji katika mikataba mbalimbali ambayo serikali inaingia na wawakezaji kutoka nje ni moja ya sababu ya kuongezeka kwa rushwa kwa baadhi ya watumishi wa umma na wawekezaji.
Hayo yamebainishwa na Mwahadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Idara ya Uchumi Profesa Humphrey Moshi wakati akizungumza na mwandishi habari hii kwenye kongamano ambalo linaratibiwa na taasisi ya Jukwaa la Sera (Policy Forum).
Alisema kukosekana kwa  uwazi katika  mikataba mbalimbali ni moja ya sababu ambayo imekuwa ichangia rushwa kwenye michakato na makubaliano mengi ambayo yanahusisha serikali na wawakezaji.
Profesa Mushi alisema Serikali imekuwa inapata kigugumizi katika kuweka wazi baadhi ya mikataba kwa kile kinachodaiwa kuwa ni siri baina ya mwekezaji na serikali jambo ambalo halina ukweli tofauti na rushwa.
“Mimi nimekuwa nikifanya tafiti mbalimbali hasa za mausuala ya kukua kwa uchumi ni wazi kuwa zipo fedha nyingi ambazo zinapotea ambapo mwanzo wake unaanzia kwenye uingia ji wa mikataba hadi katika utekelezaji  ambazo zinaelekezwa katika rushwa”, alisema Mushi.
Mwahadhiri huyo wa UDSM alisema kuonyesha kuwa serikali haina dhamira ya kuondoa hiyo changamoto imekuwa ikiwaruhusu wawekezaji hao kutoweka hata akaunti zao wazi kama ilivyo kwa nchi zingine duniani.
Profesa Mushi ambaye pia aliwahi kuwa mshauri wa masauala ya uchimi wa Rais wa Zanzibar Abeid Aman Karume pamoja na Ofisi ya Hazina ya Tanzania alisema iwapo Tanzania itajikita katika uwazi, uwajibikaji na uadilifu maendeleo yatapatikana kwa haraka.
Mchumi huyo mwandamizi alisema ni dhahiri kuwa kumekuwepo kwa ukiukwaji mkubwa katika maamuzi hivyo ni vema kujiangalia upya kwa lengo la kuleta mabadiliko chanya kwa maslahi ya Taifa.
Alisema Tanzania ni nchi ambayo imebarikiwa fursa mbalimbali ila kukosekana kwa uadilifu na uwazi kwa baadhi ya watendaji rasilmali hizo zipo hatarini kupotea.

'Leteni filamu zenu DFF 2014 mjitangaze zaidi'

https://thumbp22-ne1.mail.yahoo.com/tn?sid=2126005954&mid=AKh2imIAABCBVCU0VAAAAE%2FiWx0&midoffset=2_0_0_1_3332247&partid=2&f=1214&fid=Inbox&m=ThumbnailService&w=3000&h=3000KAMPUNI ya Haak Neel Production na Filamucentral waandaaji wa Tamasha la Dar Filamu Festival wanawakaribisha watengenezaji wote wa filamu  zinazotumia Lugha ya Kiswahili kutuma au kuwakilisha filamu zao katika ofisi za Haak Neel Production zilizopo Mikocheni kwa Mwalimu Nyerere.

TAMASHA kubwa kabisa la filamu Swahilihood hilo linapokea kazi zilizotoka mwaka 2013/2014 kwa ajili ya kuonyeshwa katika tamasha kubwa linalounganisha wadau na watengeneza filamu kutoka sehemu mbalimbali za Ulimwengu na kutoa fursa kwa wadau wengi kutengeneza soko lingine.

Akiongea na FC mkurugenzi wa Haak Neel Production Godfrey Katula amesema kuwa tamasha la mwaka huu litakuwa la aina yake kwani litafika kila kona ya Wilaya za Dar es Salaam na kutoa burudani ya kazi nzuri zinazotengenezwa na watanzania.

“Kama ilivyo kauli mbiu yetu inasema “FILAMU ZETU, MAISHA YETU” ni kauli mbiu ya kutia matumaini kwa watengenezaji na watazamaji kwani filamu tuaamini kuwa ni kazi inayoweza kutengeneza ajira kubwa kwa kila mtu,”anasema Katula.

Tamasha hili ambalo limelenga kukuza Lugha ya Kiswahili na kufanya kuwa ni biashara na alama kubwa kwa filamu zetu zinateka soko Afrika ya Mashariki kwa kuongea Kiswahili kitamu na kinzuri kinachovutia kwa wanaAfrika mashariki na Ulaya.

Mtengenezaji wa filamu au mtayarishaji  unatakiwa kuwakilisha filamu nakala mbili za filamu ambayo imetoka mwaka na kuonyeshwa kwa mwaka 2014, ikiwa samba na utambuzi wa mtayarishaji, imekaguliwa na Bodi ya Filamu pamoja na taratibu husika katika taasisi za filamu.

Kwa mawasiliano na jinsi ya kuwakilisha filamu zenu wasiliana na +2552773113, +255754 578 730, +255754 260 688 Ongea na Dada Unce anakupatia maelekezo ya kufika katika ofisi za Haak Nell Production.

NCCR-Mageuzi yalia na Wabunge wa BMK

Faustin Sungura (kulia) katika moja ya mikutano yake na wanahabari
Na Kipimo Abdallah
CHAMA cha NCCR-Mageuzi kimesikitishwa na kitendo cha Bunge Maalum la Katiba kuhitaji wajumbe ambao hawapo nchini au ndani ya Bunge kuruhusiwa kupiga kura wakati ukweli ni kwamba ushiriki wao katika utengenezaji wa rasimu hiyo ulikuwa mdogo.
Kaimu Katibu Mkuu wa NCCR-Mageuzi Faustin Sungura, aliyasema hayo juzi alipozungumza na mwandishi wa habari hii kwa njia ya simu.
Alisema utaratibu huo wa kuruhusu wajumbe walioko nje kupiga kura haujawahi kutokea katika Bunge lolote duniani jambo ambalo linatia aibu kwa Taifa.
Kaimu Katibu huyo alisema iwapo wajumbe hao ambao hawakushiriki katika mchakato kwa kiwango cha kuridhisha wataruhusiwa kupiga kura hali hiyo ingekuwa hata kwa wale wa UKAWA kwani uwepo wao nje una sababu kama hao wengine.
“Jamani Watanzania tuamke hii sasa aibu tunapopelekwa pabaya haiwezekani watu wapo nje ya Bunge alafu wapewe nafasi ya  kupiga kura jambo ambalo haliwezi kuvumiliwa kwani linatia aibu nchi”, alisema.
Alisema katika Bunge hilo linaloendelea mkoani Dodoma mambo mengi yamekiukwa ila hapo walipofikia ni vema jamii ya Kitanzania ikafungua macho na kuamua kufanya maamuzi mazito kwani kinachoonekana ni watu kuhitaji kwa maslahi yao.
Sungura alisema ni vema Wabunge waliopo Dodoma wakatambua kuwa mambo megine hayalazimishwi kwani yanahusu jamii kubwa na sio kama wanavyofikiria kuwa wao ndio wanahusika pekee.
Alisema NCCR-Mageuzi imejipanga kuhakikisha kuwa katiba hiyo inakataliwa kutokana na ukweli kuwa kilichopo ndani sio yaliyokuwa mapendekezo ya wananchi ambayo yaliwakilishwa na iliyokuwa Tume ya Katiba.
Sungura alisema ukweli dhidi ya UKAWA kutoka Bungeni umedhihirika hivyo juhudi zao ni kuhakikisha kuwa rasimu hiyo haipitishwi na wananchi kutokana na kudharauliwa kwa maoni yao ambayo walipendekeza katika rasimu ya Jaji Joseph Warioba.
Kaimu Katibu Mkuu huyo alisema nguvu yao pia inaongezwa na maamuzi ya Mahakama Kuu hivi karibuni ambapo imeweka bayana kuwa kitendo kilichofanywa na Mwenyekiti wa Bunge hilo kupokea maoni mapya ni ukiukwaji wa sheria.
Sungura alisema mabadiliko na maingizo mapya yaliyofanywa na Bunge hilo ambalo alilitaja kuwa ni la upande mmoja yamekiuka sheria kwa kiwango kikubwa na cha kusikitisha.
Alisema kwa sasa NCCR- Mageuzi ipo katika mikakati ya kuhakikisha wananchi wanapata elimu sahihi juu ya mchezo mchafu unaofanywa na Bunge hilo jambo ambalo litawajengea uwezo wa kufanya maamuzi sahihi katika upigaji kura.

Mwisho

Vyombo vya Habari vyaaswa kujenga Maadili ndani ya Jamii

http://www.thehabari.com/wp-content/uploads/2011/07/Wapigapicha.jpg
Wanahabari wakiwa kazini
Na Suleiman Msuya
RAI imetolewa kwa vyombo vya habari, taasis mbalimbali, vikundi vya kijamii, wananchi na serikali kushirikiana kwa pamoja katika kujenga jamii yenye maadili kuanzia ngazi ya familia ili kuleta maendeleo katika nchi.
Hayo yamebainishwa na Afisa kutoka IQ Management Solutions Joel Nanamka wa wakati akizungumza na MICHARAZO jijini Dar es Salaam.
Alisema iwapo kutakuwepo kwa ushirikiano baina ya sekta hizo ni wazi kuwa jamii itazingatia maadili katika suala lolote ambalo linafanyika kwa maslahi ya Taifa.
Nanamka alisema vyombo vya habari kama moja ya muhimili usio rasmi bado havijafanya kazi ya dhati ili kuweza kuibadilisha jamii ambayo inaonyesha dhahiri kupotea katika misingi ya utu.
Afisa huyo alisema ukosefu wa maadili hasa katika sekta mbalimbali za serikali kumekuwa kukichangia ukosefu wa huduma bora na zenye viwango kwa jamii.
“Kimsingi suala la kuwepo kwamaadili ni mtambuka ila kwa mtazamo wetu katika tafiti mbalimbali tunaona kuwa nafasi ya vyombo vya habari katika kufanikisha hilo ni kubwa hivyo vinapaswa kubadilika kutokana na ukweli kuwa watu wengi wanafikiwa”, alisema.
Alisema IQ Management Solutions imekuwa ikifanya juhudi mbalimbali za kuhakikisha kuwa maadili yanakuwepo kwa kanuni, sheria, zawadi na matisha pamoja na adhabu ambazo zitakuwa katika mtazamo hasi.
Kwa upande wake Afisa Programu kutoka taasisi ya Afrika Leadership Initiative Foundation Limited Alice Mwiru alisema katika kuhakikisha kuwa kunakuwepo kwa jamii yenye maadili taasisi yao imejikita kufanya kazi na vijana ambao wanaonyesha nia za kuongoza.
Mwiru alisema wao wanaamini kuwa kuwepo kwa viongozi wenye maadili ni chachu ya kuwepo kwa jamii ambayo itakuwa katika misingi hiyo.
“Sisi ALI EAF tunaamini kuwa jamii ikikuwa kwa misingi ya maadili hasa kuanzia utotoni  ni wazi kuwa kila Mtanzania atakuwa kwenye misingi hiyo kwa faida yake na nchi kwa ujumla”, alisema

Barua ya wazi kwa Wajumbe wa Bunge la Katiba kutoka Zanzibar

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhOkLsciXf-74G8GIdbS_htvzslWBy8miIPYzTL96vqTVCU_0Tg1cOReOW6eT0QjqSONTsFX3mfXtU9sxZ6p14UIXghJu9H5CZcjNo-wlAeSz-A8BWvps1Lmj_8MrM-CgwAe0rLJ8Kl2LPx/s1600/WABUNGE+WAKIPITIA+RASIMU+YA+MAPENDEKEZO+YATAKAYO+TUMIWA+NA+KIKAO+CHA+BUNGE+LA++KUJADILI++RASIMU+YA+KATIBA.JPG
Assalam alaykum
Natumai hamjambo ndugu, kaka na dada zangu. Inshallah Mwenyenzi Mungu akupeni afya na uzima kuelekea kipindi hiki muhimu cha kupiga kura kuamua Katiba Inayopendezwa na pia Mola akupeni busara na maamuzi mema.
Nakuandikieni barua hii kama Mzanzibari mwenzenu sina zaidi ya hilo. Ni kutokana na Uzanzibari wangu nimeona kuwa nijaribu kukuaidhini, kunasihini, kukushawishini, kukusemeshini, kukuombeni kuwa msiikubali Katiba Inayopendekezwa na muipigie kura ya HAPANA.
Tafadhalini wekeni mbali ushindani, itikadi na mitazamo ambayo inatutenganisha Wazanzibari na muamue kwa maslahi makubwa, mapana na ya muda mrefu ya Zanzibar. Msitizame tulipojikwaa bali tizameni tulipoanguka. Msitizame nyuma mkahesabu visa na mikasa ila nyinyi hapo mlipo ndio wenye fursa ya kuikoa, kuinusuru na kuihuisha Zanzibar.

Naam, ni kura ya HAPANA ndio ambayo itaibakisha, itaiokoa, itaisimamisha Zanzibar. Mjue mkipigia kura ya NDIYO maana yake ni kuwa Zanzibar tuipendayo inazidi kupungua, kuchukuliwa na kumezwa kama ambavyo imekuwa khofu yetu kwa miaka kadhaa ya Muungano huu.
Nataka muamini ndani ya dhati yangu mimi ni muumini wa Muungano. Nataka Muungano wa haki na hadhi sawa baina ya Washirika wa Muungano – Tanganyika na Zanzibar- ili kila nchi ipate fursa sawa za kuhudumia watu wake.
Wengi wenu kwa kauli zenu mara kadhaa mmekuwa mkisema Muungano hauakisi hali ya usawa, haki na hadhi sawa lakini mkawa mnatumia neno KERO kuwasilisha fikra zenu hizo, na wengi tukawa na matumaini kwamba fursa hiiya kuunda upya Katiba yetu itapunguza kama si kuondosha kabisa KERO hizo.
Ila baada ya kuiona Katiba inayopendekezwa nimeona kuwa andiko hilo halina msaada, halina muelekeo na halina wema na Zanzibar. Kulikubali andiko hilo ni kujitia kitanzi wenyewe na sasa imekuwa ni kusokotwa, kubanwa na kudhibitiwa Zanzibar lakini mara hii itakuwa kwa kujitakia wenyewe.

Huko nyuma tumekuwa tukisema kuwa kumekuwa na hadaa, sijui ujanja, sijui ghalat,sijui unyemela wa kuongeza Mambo ya Muungano ambayo yamekuwa yakipunguza madaraka ya Zanzibar, lakini mara hii tunajichinja wenyewe kwa mikono yetu.
Hii ilikuwa ni fursa kubwa kwetu kusimama kama Zanzibar. Zanzibar ilipaswa kusimama kama kundi zima ndani ya Bunge na kukaa na kundi zima la upande wa pili yaani Tanganyika, na watu wa pande mbili hizi kuamua umbo, hadhi na sifa gani tunataka Tanzania iwe.
Hili la pande mbili lilikuwa lisionewe aibu kwa sababu ndio ukweli na uhalisia kwamba tuko pande mbili. Haiwezekani kuwa na Muungano, ambapo upande mmoja una kila sifa za kuwa nchi, halafu upande mwengine uwe na sifa za kuwa dola na nchi ifichwe ndani yake.

Ilikuwa ni nafasi nzuri kwa Zanzibar kudai haki zake, stahiki zake, fursa zake ili iweze kukidhi mahitaji ya watu wake, maana hata kama tumo ndani ya Muungano basi bado tuna chumi mbili zinazoshindana na kwa kweli zinazopigania na kunyang’anyiana rasilmali karibu zile zile.
Ilikuwa ni wakati wa kufanya kila njia ili Zanzibar ijitengenezee fursa ya kuwa na mafanikio kama ya Visiwa vya Seychelles au Mauritius ambavyo wastani wa kipato cha mwananchi wa nchi hizo mbili ni zaidi ya dola 14,000 na dola 15,000 mtawalia.
Najua hoja itakuja basi haya yangefanywa kwa umoja, na mbona umoja huo haukuwepo, nakiri kuwa hilo kweli limetokea, lakini ni kama katika mchezo iwapo mchezaji mmoja ametolewa ama kwa kuonewa na mwamuzi au kwa kitendo chake cha makusudi, haina maana kuwa waliobakia uwanjani wakubali kupoteza mchezo, badala yake hujibidiisha kushinda ili iwe njia moja ya kumsuta mwenzao aliyetolewa na sifa kwa kweli inakuja kwa waliobakia uwanjani.
Kwa kuendelea kujigandisha katika ubavu, kuendelea kuamini kuwa hatuwezi kujitegemea na kwa hivyo mambo kadhaa kuyabakisha katika Muungano ni kujiviza akili, ni kujidhalilisha kimkakati na kujidogosha kihadhi.
Si kweli na si kweli kabisa kuwa Katiba Inayopendekezwa ina maslahi na Zanzibar. Haina, haina katu, haina Abadan, kamwe haina. Ni katiba ambayo inatuweka pabaya na pagumu zaidi na imeendelea kuyachukua mamlaka ya Zanzibar na kuyatia katika Muungano.

Vipi Katiba hii itakuwa na maslahi na sisi? Hebu tutizame mambo machache:
1. Kundosha au kuukataa mfumo wa Shirikisho ina maana
a) Zanzibar haiwezi kuwa na hadhi na haki sawa na Serikali ya Muungano.
b) Tumejibakisha pale pale Zanzibar haina mshirikia mwenziwe kwenye Muungano
c) Tumerudi pale pale mshirika wa Zanzibar ni Tanzania na kwa hivyo hakuna usawa
d) Tumeganda pale pale kuwa Tanganyika inasimamiwa na Serikali ya Muungano
e) Tumesalia papo kuwa Bunge la Muungano linatunga sheria za Tanganyika na tunajua kuwa sheria kama hizo hazina nguvu Zanzibar
f) Tumejizuga vile vile kumwita Waziri wa Muungano hata asiesimamia jambo la Muungano kama kilimo bila ya kuwa na hadhi kama hiyo.
g) Tumekwama pale pale Mahakama Kuu ya Tanganyika inaitwa ya Muungano
h) Tumejidanganya vile vile wafanyakazi wote wa Tanganyika wanabaki ni wa Muungano na wale wa Zanzibar mwisho wao Chumbe.

Fikiria hii ndio Zanzibar tuitakayo?
2. Tunajipa moyo kuwa kumfanya Rais wa Zanzibar kuwa ni Makamo wa Rais wa Muungano kuna manufaa kwa Zanzibar ilhali hakutakuwa na msaada wowote.
Tumewapa watu matumaini kuwa hilo litawezesha Rais wa Zanzibar akitoka nje atakuwa na hadhi ya kimuungano wakati tunajua hilo litaleta utata mkubwa zaidi huko mbele. Kwanza kwa suala la gharama pili kutakuwa na mgongano wa maslahi na majukumu yake kama Rais wa Zanzibar vs Umakamo wa Muungano

3. Haiwezekani Rasimu Inayopendekezwa iwe imenyofoa mamlaka zaidi yaliokuwa yameanza kuikaribia Zanzibar kutokana na Rasimu ya Warioba, halafu isemwe kuwa kuna maslahi kwa Zanzibar.
a) Kuondoa uwezo wa Zanzibar kuunda Benki yake
b) Kurudisha nguvu za kuigawa Zanzibar kwa Rais wa Muungano
c) Kukubali ardhi kurembwa
d) Tumerudisha suala la Tume ya Pamoja ya Fedha ambayo imeshindikana kwa miaka kadhaa toka nia hiyo ilipotiwa kwenye Katiba ya 1977.
4. Uamuzi wa kuyatia madaraka ya Serikali ya Zanzibar ndani ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano ilhali hakuna sehemu yoyote ya Katiba Inayopendekezwa ambapo madaraka ya Serikali ya Tanzania Bara kama inavyoitwa yameainishwa ni kuendelea kujidanganya.

Pili, kwa kufanya hivyo tunarudi tena pale pale ambapo Zanzibar inaonekana inakiuka Katiba ya Jamhuri pale inapotaka kufanya mabadiliko yenye maslahi yake, ilhali jambo kama hilo halionekani na wala halipo kwa upande wa mshirika mwenziwe, maana mshirika ni huyo huyo Serikali ya Jamhuri na Serikali ya Tanzania Bara.
Ndugu, kaka na dada zangu ujue wazi kuwa maamuzi unayotaka kuyafanya ni makubwa na yana athari ya muda mrefu kwa vizazi vingi vya Zanzibar, ambayo pamoja na tofauti zetu, lakini naamini tunakubaliana kuwa Zanzibar tuipendayo iwepo. Na kuwepo kwake lazima iwe na nguvu na matao yake.
Na kwa dalili zote Rasimu Inayopendekezwa inapopotoa nguvu na matao ya Zanzibar. Inaondosha uzuri na haiba yake kwa kuifanya kuwa ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano badala ya kuwa ni nchi moja kamili ndani ya Muungano huu.

Fikirini, pimeni na muvuke nje ya itikadi na mitizamo. Fanya uamuzi ili nafsi yake iwe na amani kwa sababu umefanya uamuzi wako bila ya shindikizo, maelekezo au utashi wa kisiasa, maana wewe kwanza ni Mzanzibari kisha mengine ndio yanafuata.
Nawaomba radhi kwa uamuzi huu wa kuandika barua ya wazi maana isingewezekana kumfika kila mmoja wenu, lakini nataka muamini kuwa barua hii nimeiandika kwa sababu nimeona kuna wajibu kwangu kufanya hivyo.
Unapotaka kupiga kura fikiria, wazia na pimia juu ya uzito wa mchoro wako mmoja tu wa kalamu utavyokuwa na athari kwa nchi yako, watu wako na watoto na wajukuu wako. Fumba macho, rudisha nyuma fikra zako,
kumbubuka wema na ihsani za waliokuzunguka, uliokuwa nao pamoja katika maisha yako na uwafikirie khatma njema ya muda mrefu.

Kumbubuka jukumu lako kwa Mwenyenzi Mungu na fikiria kama hicho ni kitendo cha mwisho cha maisha yako ili ukitie katika mizania nzuri ya maamuzi yako.
Piga HAPANA kwa faida ya Zanzibar na usinitizame mimi kama Ally Saleh, la. 

Mimi ni mtu mmoja tu tena tunaweza kuwa tuna mzigo wa tofauti zetu, lakini pamoja na yote mimi na wewe ndio Zanzibar.
Kwa maslahi ya Zanzibar piga HAPANA.

Ally Saleh
Zanzibar

Kocha Liverpool akiri Balotelli bado sana, japo amemsifu Anfield

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhz4XqJAAKnprDJap4_tn1QZtE-90nE7JVa1KXPPSo34ulgKddta1D1UPbRVLDhilRX1FxRY0gMqnVBAMwH97o56EtYPXHAVmH_AE1iGygVEZivYIp7SRNaIE-ui9fyJ4BEMaiUxyiG8m5u/s1600/baloooooooooo.jpgMENEJA wa klabu ya Liverpool, Brendan Rodgers amekiri kuwa Mario Balotelli bado hajafikia hadhi ya kiwango cha dunia lakini amemuunga mkono kuwa anaweza kuvaa viatu vya Luis Suarez na kufanya vitu vikubwa Anfield. 
Suarez aliuzwa Barcelona kwa kitita cha euro milioni 88 katika usajili wa kiangazi huku nafasi yake ikizibwa na Balotelli aliyesajiliwa akitokea AC Milan kwa kitita cha euro milioni 20. 
Rodgers anaamini kuwa nyota huyo wa kimataifa wa Italia anapswa kufuata nyayo za Suarez akiwa hapo na kuonyesha thamani yake akiwa kama mshambuliaji. 
Rodegrs amesema pamoja na kwamba Balotelli hajafikia hadhi ya kiwango cha dunia lakini hana shaka na kipaji chake kwani ana uwezo wa kufikia huko kama akitilia maanani kazi yake hiyo.

Nasibu Ramadhani, Moh' Matumla kumaliza ubishi leo Manzese

  MABONDIA Nasibu Ramadhani na Mohammed Matumla wakitunishiana misuli jana wakati wakipimwa uzito. Mabondia hao wanatarajiwa kuonyeshana kazi leo kwenye ukumbi wa Friends Corner -Manzese Dar.
Mratibu wa mpambano wa ngumi Ibrahimu Kamwe katikati akiwangalia mabondia wa kike Lulu Kayage kushoto na Fatuma Yazidu wanavyo tunishiana misuli baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao
Lulu Kayage na Fatuma Yazidu wakitambiana baada ya kupima uzito
Bondia Nassibu Ramadhani akipima uzito kwa ajili ya mpambano wake na Mohamedi Matumla

Mohamed Matumla akipima uzito
Bondia Nassibu Ramadhani na Mohamed Matumla wakinuliwa mikono juu na Mratibu wa mpambano huo Ibrahimu Kamwe katikati  mpambano utakaofanyika leo Jumamosi hii katika ukumbi wa Friends Corner Manzese
Bondia Juma Fundi na Issa Omari wakinuliwa mikono juu na Mratibu wa mpambano huo Ibrahimu Kamwe katikati  mpambano utakaofanyika jumamosi hii katika ukumbi wa Friends Corner Manzese
Bondia Lulu Kayage akipimwa na Daktari baada ya kupima uzito kushoto ni mpinzani wake Fatuma

Kocha Mkwasa apata ulaji TFF baada ya kurejea umangani

ALIYEKUWA kocha wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa 'Master' ameteuliwa kuwa Ofisa Mtaalamu wa Elimu ya Mafunzo wa Shirikisho la Soka Tanzania, TFF.
Katibu wa TFF, Selestine Mwesigwa ameithibitisha juu ya Mkwasa kupewa nafasi hiyo baada ya kurejea kutoka Uarabuni, alipokwenda kufundisha klabu.  
Kwa upande wake, Mkwasa, amesema kuwa amekwishaanza kazi yake hiyo mpya TFF na anatarajia kuifanya kwa ufanisi kwa sababu ana utaalamu nayo.
Juu  ya mkataba wake na Yanga, Mkwasa alisema kwamba wakati anakwenda Uarabuni alipewa likizo ya mwaka mmoja, kwa sababu amerudi kabla ya muda huo ameona bora kukubali kazi hiyo ya TFF kuliko kukaa bure.  
“Kama Yanga SC watanihitaji kurudi kazini kabla ya muda huo, ni suala la kuzungumzika tu, kwa sababu TFF ipo kwa ajili ya maendeleo ya soka hapa nchini na Yanga ni klabu ya Tanzania,” amesema Mkwasa.
Mkwasa alijiunga na Yanga Desemba mwaka jana akitokea Ruvu Shooting ya Pwani, lakini baada ya msimu Mei mwaka huu akaondoka pamoja na aliyekuwa kocha Mkuu wa klabu hiyo, Mholanzi Hans va der Pluijm kwenda Uarabuni.  
Hata hivyo, baada ya muda mfupi wa kufanya kazi huko, Pluijm aliyemchukua Mkwasa kwenda naye huko- akatofautiana na uongozi wa timu na kusitishiwa mikataba.