STRIKA
USILIKOSE
Friday, August 3, 2012
Ngassa hatimaye akubali kutua Simba, wanachama wasubiri maelezo mkutano wa Jumapili
NYOTA wa kimataifa wa klabu ya Azam na Taifa Stars, Mrisho Ngassa ambaye juzi alinukuliwa kuigomea klabu yake kumpeleka Simba, hatimaye mchezaji huyo ameridhia kwenda mwenyewe Msimbazi baada ya kuahidiwa mambo mazuri katika klabu hiyo mpya.
Hata hivyo kuna taarifa kwamba licha ya uongozi wa Simba kufanikiwa kumweka sawa mchezaji huyo, baadhi ya wanachama wamekuwa na mashaka na mchezaji huyo wakiamini ni mnazi mkubwa wa Yanga na hivyo watatoa hatma yake kwenye mkutano wa wanachama utakaofanyika siku ya Jumapili.
Baadhi ya wanachama wa klabu hiyo waliiambia MICHARAZO kwamba hawaamini kama Ngassa atacheza kwa mapenzi katika timu yao na pia kuhoji uongozi kitu gani kilichoufanya umchukue mchezaji huyo.
Ngassa alinukuliwa jana kuwa yu tayari kuichezea Simba kwa vile yeye hana mapenzi na klabu yoyote zaidi ya kulitumikia soka na mchana huu alitarajiwa kutambulishwa rasmi na uongozi huo kwa waandishi wa habari.
Winga huyo aliyewahi kung'ara na timu za Toto Afrika, Kagera Sugar na Yanga kabla ya kwenda Azam, ametua Simba kwa mkopo ikidaiwa kalipwa kiasi cha Sh. Milioni 30 na gari aaina ya Verosa na atakuwa kilipwa mshahara wa Sh Milioni2 kwa mwezi.
Pamoja na sakata la mchezaji huo kuonekana limeisha baada ya Azam na Simba kumalizana kufuatia Yanga kushindwa katika mbio za kumwania kumrejesha Jangwani, wanachama wa Simba wamesisitiza kuwa uongozi wao unapaswa kuwapa majibu ya kuridhisha katika mkutano wao siku ya Jumapili.
Mmoja wa wanachama hao ambao yupo kwenye baraza la wazee wa klabu hiyo (jina tunalo) alisema wameshangazwa na uongozi wao kumnyakua Ngassa kabla hata hawajalimaliza sakata la beki wao Kelvin Yondani aliyetimkia Yanga, huku ikidaiwa ana makataba nae.
"TUnajua soka ndivyo lilivyo, lakini naamini Ngassa anaweza asicheze kwa kiwango chake kama alivyo kwa sababu ya watu kumhisini ana uyanga, ila viongozi wajiandae Jumapili kutueleza kilichotokea na namna Yondani alivyotukimbia," alisema mwanachama huyo.
Kelvin Yondani, aliyekuwa akituhumiwa kuwa mnazi wa Yanga, aliitema Simba mara baada ya kumalizika kwa ligi kuu msimu uliopita na kutua Yanga ambapo aling'ara kwenye michuano ya Kombe la Kagame.
Pengo la Yondani lilionekana wazi kwenye kikosi cha Simba kilichotolewa hatua ya robo fainali kwa kunyukwa mabao 3-1 na Azam.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment