|
Bondia
Fransic Cheka akinyooshwa mkono juu na mmoja wa mashabiki wa Kigeni
waliokuja kuangalia mpambano wake dhidi ya Karama Nyilawila Cheka
alishinda katika raundi ya sita baada ya karama kusalimu amri kushoto ni
Rais wa PST Emanuel Mlundwa na wa pili kulia ni mgeni rasmi Kamanda wa
polisi wa Kanda Maalumu Mkoa wa Dar es salaam Suleiman Kova.Picha na
www.superdboxingcoach.blogspot.com |
|
Refarii wa mpambano akiwaelekeza mabondia wasicheze kwa kukumbatiana |
|
Bondia
Fransic Cheka kushoto akipepesuka baada ya kupigwa ngumi na Karama
Nyilawila wakati wa mpambano wao uliofanyika usiku wa jumamosi cheka
alishinda kwa K.O raundi ya sita na kufanikiwa kunyakuwa ubingwa picha
na www.superdboxingcoach.blogspot.com |
|
Bondia
Fransic Cheka kushoto akimshambulia Karama Nyilawila kwa masumbwi
wakati wa mpambano wao uliofanyika usiku wa jumamosi Cheka alishinda
raundi ya sita baada ya kumpiga na kudondoka chini baada ya kuesabiwa
akashindwa kuendelea picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com |
|
Bondia
Karama Nyilawila kulia akijitaidi kukwepa makonde ya mpinzani wake
Fransic Cheka wakati wa mpambano wao uliofanyika usiku wa jumamosi cheka
alishinda kwa K,o raundi ya sita picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com |
|
Mabondia
Karama Nyilawila kushoto akionesheana umwamba wa kutupa masumbwi na
Fransic Cheka wakati wa mpambano wao cheka alishinda kwa K,O Raundi ya
sitapicha na www.superdboxingcoach.blogspot.com |
|
Fransic
Cheka kushoto na Karama Nyilawila wakiwa uringoni kuoneshana uwezo wa
kutupiana masumbwi Cheka alishjnda kwa K,O ya Raundi ya sita picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com |
|
Mabondia
Karama Nyilawila kushoto na Fransic Cheka wakionesheana umwamba wa
kutupiana makonde wakati wa mpambano wao uliofanyika usiku wa jumamosi
katika ukumbi wa PTA Sabasaba Cheka alishinda kwa K,o raundi ya sita picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com |
|
Bondia Fransic Cheka akinyooshwa mkono juu na mmoja wa
mashabiki wa Kigeni waliokuja kuangalia mpambano wake dhidi ya Karama
Nyilawila Cheka alishinda katika raundi ya sita baada ya karama kusalimu
amri kushoto ni Rais wa PST Emanuel Mlundwa na wa pili kulia ni mgeni
rasmi Kamanda wa polisi wa Kanda Maalumu Mkoa wa Dar es salaam Suleiman
Kova.Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com |
|
Bondia Fransic Cheka akinyooshwa mkono juu na mmoja wa
mashabiki wa Kigeni waliokuja kuangalia mpambano wake dhidi ya Karama
Nyilawila Cheka alishinda katika raundi ya sita baada ya karama kusalimu
amri kushoto ni Rais wa PST Emanuel Mlundwa na wa pili kulia ni mgeni
rasmi Kamanda wa polisi wa Kanda Maalumu Mkoa wa Dar es salaam Suleiman
Kova.Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com |
|
Bondia Fransic Cheka akinyooshwa mkono juu na mmoja wa
mashabiki wa Kigeni waliokuja kuangalia mpambano wake dhidi ya Karama
Nyilawila Cheka alishinda katika raundi ya sita baada ya karama kusalimu
amri kushoto ni Rais wa PST Emanuel Mlundwa na wa pili kulia ni mgeni
rasmi Kamanda wa polisi wa Kanda Maalumu Mkoa wa Dar es salaam Suleiman
Kova.Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com |
BINGWA wa ngumi za kulipwa anayetambuliwa na vyama vya ICB, IBF na WBC, Francis Cheka 'SMG' usiku wa kuamkia leo amedhihirisha kwamba hana mpinzani katika ngumi hizo nchini baada ya kumchapa kwa KO mpinzani wake mkubwa, Karama Nyilawila na kuongeza taji jingine.
Cheka alimpiga Nyilawila katika raundi ya sita ya pam,bano hilo lililokuwa la uzani wa Super Middle la raundi 12 lililofanyika kwenye ukumbi wa PTA, Temeke jijini Dar es Salaam na kutwaa ubingwa wa Mabara wa UBO uliokuwa wazi.
Pambano hilo lililohudhuriwa na mashabiki lukuki, lilishuhudia raundi zote tano za kwanza Nyilawila akionyesha kumdhibiti Cheka kwa kumchezea 'kibabe' akitumia nguvu nyingi kujihami na baadhi ya watu ukumbini kuamini mwisho wa tambo za Cheka zilikuwa zimewadia.
Hata hivyo raudni ya sita ilipoanza Cheka alionyesha amebadilika na hasa baada ya kocha wake Abdallahj Saleh 'Komando' kupanda ulingoni na kuzungumza na bondia huyo na kumshushia kipigo Nyilawila, ambapo moja ya makonde matatu ya mfululizo yalimpeleka chini mpinzani wake.
Mwamuzi wa pambano hilo, Jerome Waluza alimhesabia Nyilawila ambaye alijitahidi kuinuka, lakini ghafla akaonyesha ishara kwamba asingeweza kuendelea na pambano hilo na ukumbi mzima kuripuka kwa shangwe akishangiliwa Cheka ambaye hiyo ni mara ya pili kumpiga Nyilawila.
Kabla ya pambano hilo lililoanza majira ya saa 3;40 usiku, kulikuwa na mapambano saba ya utangulizi pamoja na burudani ya muziki toka bendi ya Mashujaa ambao hata hivyo sio wapenzi wengi walioweza kuishuhudia kutokana na kuondoka ukumbini mapema.
Katika pambano la kwanza la utangulizi Said Mbelwa alimpiga kwa pointi Dickson Mwakipesile, Juma Kihiyo alipigwa kwa pointi na Ibrahim Mahokola katika pambano lililovutia kwa namna mabondia hao walivyoonyeshana kazi.
Pia mdogo wa Cheka, Cosmas Cheka alifanikiwa kuibuka na ushindi wa pointi dhidi ya Fadhil Awadh katika pamnbano jingine lililosisimua wengi kwa ufundi uliokuwa ukionyesha na mabondia hao, naye Shaaban Kilumbelumbe alimpiga kwa pointi Anthony Mathias kabla ya Safari Mbiyu kumpiga kwa KO ya raundi ya kwanza Khalfan Jumanne.
Michezo minginme iliwakutanisha Stan Kessy na Seba Temba, pambano lililoisha kwa mabondia hao kutoka sare na Hassani Kidebe alitolewa nishai na Deo Samwel kwa kupigwa kwa pointi.
Mgeni rasmi katika pambano hilo alikuwa Kamanda wa Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam ambaye aliutangazia umma kwamba kama Mlezi wa Ngumi za Kulipwa amefanikiwa kuwafuta wafadhili katika mchezo huo na kumtambulisha raia mmoja wa kigeni kwamba ni miongoni mwao.
No comments:
Post a Comment