STRIKA
USILIKOSE
Monday, December 31, 2012
Julio afichua siri Msimbazi
KOCHA msaidizi wa timu ya vijana chini ya miaka 17 Serengeti Boys, Jamhuri Kihwelo 'Julio', aliyerejeshwa Msimbazi kama kocha msaidizi, amefichua siri ya wachezaji wa Simba akidai wengi wao wana matatizo ya kutokuwa na pumzi na stamina ya kutosha.
Julio, alisema kutokana na kupewa jukumu la kuwanoa vijana hao kama kocha wa viungo wa Simba atarekebisha tatizo, ili timu yao iweze kufanya vema katika duru lijalo la ligi kuu pamoja na uwakilishi wa nchi kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Beki huyo wa zamani wa Simba na Taifa Stars, alisema pamoja na mambo mengine yaliyoiponza Simba kwenye duru lililopita, amegundua tatizo kubwa kwa kikosi hicho ni kukosekana kwa stamina na pumzi za kutosha kwa nyota wa timu hiyo.
Alisema kutokana na kubaini tatizo hilo, amejipanga kuwanoa wachezaji hao ili wawe 'ngangari'.
Julio alisema anadhani tatizo hilo ndilo lililoigharimu Simba kwenye duru la kwanza kwa wachezaji wake kushindwa kumudu dakika zote 90 za mchezao badala yake kuonekana tishio dakika 45 za kwanza na kuwa 'urojo' dakika 45 za pili na kupata matokeo mabaya.
"Nimegundua wachezaji wengi wa Simba wana tatizo la pumzi na stamina, hivyo nitajitahidi kurekebisha tatizo kabla ya kuanza kwa duru la pili la ligi ili vijana wawe ng'ang'ari," alisema.
Julio amerejeshwa Msimbazi sambamba na aliyekuwa kocha mkuu wa zamani wa timu hiyo, Moses Basena ili kumsaidia kocha mpya wa klabu hiyo, Patrick Liewig anayechukua nafasi ya Mserbia , Circokiv Milovan aliyetupiwa virango Simba.
Kwa sasa Julio na vijana wake wanaendelea kujifua kwa mazoezi ya ufukweni wakati wakisubiri kuanza kufanya mazoezi ya uwanjani mara atakapowasilia kwa Mfaransa Liewig, aliyepewa mkataba wa muda mrefu ili 'kupimwa' kiwango chake.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment