YANGA, PRIME TIME WAINGIA MKATABA
Klabu
ya Young Africans leo imeingia mkataba na kampuni ya Prime Time
Promotions ya jijini Dar es saaalm kwa ajili ya kuandaa shuguli za
mkutano mkuu wa wanachama utakaofanyika Januari 19, 2013 ambapo kampuni
ya Prime Time imetoa mil 105,000,000 kwa ajili ya kuratibu shughuli
hiyo.
Akiongea
na waandishi wa habari, makamu mwenyekiti wa klabu ya Yanga Clement
Sanga amesema wamefikia hatua hiyo kuipa nafasi kampuni ya Prime Time
kuweza kuuendesha mkutano huo kisasa zaidi, ambapo unategemewa kufanyika
na kuonyesha moja kw amoja (live) kupitia kituo cha Luninga ya Clouds.
Prime
Time pia imepewa fursa ya kusaka masoko na wadhamini wa klabu ya Yanga
ili kuhakikisha klabu inajijenga vizuri kiuchumi kwa kubuni miradi mbali
mbali, ambapo kwa kuanzia itaanda mchezo mmoja wa kirafiki na timu
kubwa barani Afrika mwanzoni mwa mwezi Januari 2013.
Naye
Mkurugenzi wa Prime Time Promotions Joseph Kusaga amesema amefurahishwa
kwa kampun yake kupewa nafasi hiyo na kusema wanaahidi watafanya kazi
nzuri kufikia malengo yaliyokusudiwa.
Aidha
Kusaga alisema milango iko wazi kwa timu yoyote kuomba kushirikiana
nao, kwani hawana itikadi ya timu yoyote bali lengo lao ni kufanya timu
zote ziwe katika nafasi nzuri kiuchumi na kujitangaza kimichezo na
kimasoko.
CHANZO:BIN ZUBEIRY
No comments:
Post a Comment