STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, February 12, 2013

Maskini Malinzi atupwa uchaguzi wa TFF


KATIBU Mkuu wa zamani wa Yanga na aliyeekuwa mgombea wa nafasi ya Urais katika Uchaguzi Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania, TFF, Jamal Malinzi ametupwa katika kinyang'anyiro hicho kinachoitarajiwa kufanyika Februari 24.

Kuenguliwa kwa Malinzi, kunaifanya nafasi hiyo ya kusaka mrithi wa Rais wa sasa wa TFF, Leodger Tenga kusaliwa na mgombea mmoja pekee ambaye ni Makamu wa Rais, Athuman Nyamlani.
Malinzi (kulia) alipokuwa akirejesha fomu za kuwania urais wa TFF
Uamuzi wa kumuengua Malinzi umetolewa jana na Kamati ya Rufaa ya Uchaguzi ya shirikisho hilo iliyokuwa ikipitria pingamizi mbalimbali ambapo Nyamlani alisalimika baada ya kuonekana kuwa utumishi wake serikalini haumzuii kuwa mgombea.
Wengine walioenguliwa ni Michael Wambura aliyekuwa akigowania nafasi ya Makamu wa Rais na Ahmed Yahya aliyekuwa akiwania nafasi ya uenuekiti wa Bodi ya Ligi.
Imeelezwa kuwa Malinzi ameenguliwa kwa sababu ya kukosa uzoefu katika uongozi.
Akizungumza jana baada ya kupata taarifa hiyo, Malinzi alisema kuwa amechoshwa na vikwazo.
Malinzi ambaye katika uchaguzi wa mwaka 2008 alipitishwa kuwa mgombea akichuana na rais wa sasa anayemaliza muda wake, Leodgar Tenga, alinukuliwa jana akisema amechoshwa na pingamizi na vikwazo ambavyo amewekewa kuhusiana na mchakato huo wa kuwania cheo hicho cha juu.
Alisema mapema jana kabla ya kutangazwa rasmi kwa maamuzi hayo kuwa ataheshimu maamuzi yatakayotolewa na kamati hiyo kwa sababu lengo lake la kuwania uongozi TFF ni kutaka kutoa mchango wake katika kuendeleza soka la Tanzania ambalo bado wadau wana kiu ya kupata mafanikio.
"Nimechoka na hali inavyoendeshwa, mimi siendi kuomba kazi, siendi kuomba ajira, siendi kufanya biashara, lengo langu ni kutoa mchango wangu katika kusukuma soka letu," Malinzi ambaye pia ni mwenyekiti wa Chama cha Soka cha Mkoa wa Kagera (KRFA) alisema.
Alisema kwamba moja ya sababu zilizomfanya awanie nafasi hiyo ni kutokana na uzoefu alionao.
Malinzi aliwekewa pingamizi na baadaye kukatiwa rufaa na Agape Fue dhidi ya Kamati ya Uchaguzi TFF kupinga kumpitisha akisema kwamba kiongozi huyo hana uzoefu.

No comments:

Post a Comment