Zoezi la kusaka miili zaidi ya watu likiendelea kufanywa kwa umakini mkubwa |
Mojawapo ya magari kibao yaliangukiwa pia na jengo hilo |
Wengine walikuwa ndani ya magari yao wakati mjengo ukiporomoka na kuwafunika |
Idadi ya miili ya watu walionasuliwa kutoka katika kifusi cha jengo la ghorofa 16 lililoporomoka juzi wakati likiendelea kujengwa kwenye makutano ya Morogoro Road na Indira Gandhi sasa imefikia 29, imefahamika.
"Hadi sasa tumeshapata miili ya watu 29 kutoka kwenye kifusi cha mabaki ya jengo lililoanguka," Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick amesema leo Machi 31, 2013.
Ameongeza kuwa waokoaji sasa wanaendelea kusaka miili zaidi katika lililokuwa jengo la chini ambako kulikuwa na ghala la vifaa na inadhaniwa kuwa huko ndiko kulikokuwa na watu wengi zaidi; na kwamba zoezi la kusaka miili litaendelea mpaka wahanga wote wapatikane.
Rais Jakaya Kikwete, ambaye alitembelea eneo la tukio juzi katika siku ya Ijumaa Kuu, ameagiza kwamba wahusika wote waliosababisha maafa hayo wafikishwe mbele ya mkono wa sheria na hadi sasa, polisi wamesema kuwa tayari wameshawatia mbaroni watuhumiwa wanne.
No comments:
Post a Comment