MABONDIA wa Afrika ya Kusini Jeffrey Mathebula na Takalani Ndlovu watakutana katika ukumbi wa Carnival City Casino jijini Johannesburg jimbo la Gauteng nchini Afrika ya Kusini katika pambano la mchujo (Elimination Title) la ubingwa wa dunia uzito wa unyoya (Featherweight).
Jeffrey Mathebula (kushoto) na Takalani Ndlovu (kulia) katika moja ya mapambano yao
Wawili
hawa ni mahasimu wakubwa wanaojulikana nchini Afrika ya Kusini na
walishakutana mara mbili ambapo Ndlovu alishhinda pambano la awali huku
Mathebula akishinda pambano la mwisho.
Wakati huo huo mabondia Vusi Malinga wa
Afrika ya Kusini na Diarh Gabutan wa Phillipines watakutana katika
mpambano mwingine wa mchujo kuwania tiketi ya kukutana na bingwa wa
dunia katika uzito wa Bantam.
Promota
maarufu wa Afrika ya Kusini Branco Milenkovic wa kampuni ya Branco
Boxing Promitions atakuwa ndiye mwandaaji wa mpambano huo utakaofanyika
tarehe 23 mwezi wa tatu mwaka huu.
Huu
ni mwendelezo wa Shirikisho la Ngumi la kKmataifa IBF katika programu
yake ua “Utalii wa Michezo” barani Afrika ambapo imejiwekea lengo la
mapambano 100 ya ubingwa mwaka huu.
No comments:
Post a Comment