Mwili wa marehemu Nyaga poul Mawalla ukiwa katika kanisa la Kilutheri nchini Kenya usharika wa Uhuru Highway kwa ajili ya misa
SHUKRANI FATHER KIDEVU
Mbunge wa Jimbo la Arusha mjini Chadema ni miongoni mwa waombolezaji waliokuwa kanisani nchini Kenya.
Mwenyekiti
wa Chadema Freeman Mbowe,Naibu Waziri wa Utalii na Maliasili Lazaro
Nyarandu na Sir George kahama wakiwa kanisani wakishiriki misa ya maziko
ya marehemu Nyaga Mawalla.
****
Mazishi
ya Marehemu Nyaga Mawalla, aliyekuwa Mwasisi na Mkurugenzi wa Makampuni
ya Mawalla ya Jijini Arusha yamefanyika jana jijini Nairobi Kenya katia
Makaburi ya Jumuia ya Langata.
Mapema
kabla ya Mazishi hayo yaliyohudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Serikali
na familia na marafiki ilifanyika Misa ya kumuombea Marehemu katika
Kanisa la KKKK, Uhuru Highway.
Miongoni
mwa Viongozi waliohudhuria Mazishi hayo ni Balozi wa Tanzania nchini
Kenya, Dk. Batilda Burian, Viongozi wastaafu, Sir. George Kahama,
Mwemyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, Wabunge, Mawaziri wanasheria
mabalimbali wa ndani na nje ya Tanzania.
Marehemu Nyaga Paul Mawalla alifariki Machi 22, 2013 jijini Nairobi alikokuwaa amelazwa kwa matibabu Hospitali ya Nairobi.
Balozi wa
Tanzania nchini Kenya Dkt Batilda Buriani akiwa na mwanasheria maarufu
Jijini Arusha anayemiliki kampuni ya uwakili ya Law /Access Advocates
Mosses Mahuna wakiwa nje ya kanisa la Lutherani nchini Kenya.
Mbunge wa
Jimbo la Simanjiro wilani Simanjiro mkoani Manyara Christopher Ole
Sendeka na Waziri wa zamani wa mambo ya ndani Laurence Marsha wakiwa
kanisani nchini Kenya maziko ya marehemu Poul Mawalla
Kiongozi wa Dini wa Kanila la Kilutheri Kenya la Uhuru Highway akiongoza Mazishi.
Sir George Kahama na mkewe wakiweka shada la maua katika Kaburi la Marehemu Nyaga Mawalla.
Familia ya Marehemu Nyaga Mawalla wakiwa wenye simanzi nzito wakati wa Mazishi hayo.
Jaji Mark bomani nae alikuwa ni miongoni mwa waombolezaji walioshiriki mazishi hayo.
Baadhi ya jamaa wa karibu wa Marehemu Nyaga ambao ni wabunge wakiweka Shada la Maua
Mwenyejiti wa Chadema, Freeman Mbowe na mkewe wakiweka shada la maua
Wabunge na Mawaziri mbalimbali wa serikali ya Jamhurti ya Muungano wa Tanzania, wakiweka mashada ya maua.
Wanafamilia wakiweka mashada ya maua
Watoto wa Marehemu Nyaga wakiwa na ndugu zao.
Balozi wa Tanzania nchini Kenya, dk. Batilda Buriani akiweka shada la maua katika kaburi la marehemu Nyaga.
No comments:
Post a Comment