Hamis Kiiza alipokuwa akiwania mpira na beki wa Mgambo JKT juzi kwenye uwanja wa Mkwakwani Tanga |
Na Boniface Wambura
PAMBANO la Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Mgambo Shooting na Yanga lililochezwa jana (Aprili 17 mwaka huu) Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga limeingiza kiasi cha sh. 24,865,000 kutokana na watazamaji 4,386.
Viingilio
katika mechi hiyo namba 162 iliyomalizika kwa timu hizo kutoka sare ya
bao 1-1 vilikuwa sh. 10,000 kwa jukwaa kuu na sh. 5,000 huku kila klabu
ikipata mgawo wa sh. 5,547,337.50 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani
(VAT) iliyolipwa ni sh. 3,792,966.10.
Asilimia
15 ya uwanja sh. 2,820,680.08, msimamizi wa kituo sh. 120,000, kamishna
wa mechi sh. 90,000, waamuzi sh. 270,000, maandalizi ya uwanja sh.
100,000 na tiketi sh. 1,587,500.
Mgawo
mwingine ni gharama za mechi sh. 1,692,408.05, Kamati ya Ligi sh.
1,692,408.05, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 846,204.05
na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Tanga (TRFA) sh. 658,158.69.
No comments:
Post a Comment