WATUHUMIWA 60 wa vurugu kati ya machinga na polisi mjini Iringa akiwemo Mbunge
wa Jimbo hilo, Mchungaji Peter Msigwa, kwa sasa wanafanyiwa
utaratibu wa dhamana baada ya mahakama kukubali kupewa dhamana.
Awali watuhumiwa walisomewa mashitaka matatu huku mbunge akisomewa
shitaka la kushawishi watuhumiwa hao kufanya vurugu.
Watuhumiwa
wote wamekana mashitaka dhidi yao na kwa sasa utaratibu wa dhamana
unafanyika mbele ya mahakama ya hakimu mkazi wa wilaya ya Iringa,
Mheshimiwa Godfrey Isaya.
Mashitaka
waliyosomewa watuhumiwa ni pamoja na shitaka la kwanza la mbunge ambalo
ni kushawishi kufanya vurugu, huku wengine wote makosa yao yakiwa ni
kufanya mkutano bila kibali, kuharibu mali kinyume na sheria ni
kufanya vurugu.
No comments:
Post a Comment