Dk Slaa (kulia) na mchumba wake, Josephine Mushumbuzi |
HATIMAYE Mahakama ya Wilaya ya
Kinondoni, imetupilia mbali rufaa iliyokuwa imekatwa na aliyekuwa mume
wa Josephine Mshumbusi, ambaye ni mchumba wa Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk Wilbroad Slaa, Mahimbo baada ya kuiona rufaa hiyo haina msingi
wowote kisheria.
Hukumu hiyo ya rufaa ya madai ya
ndoa Na.32/2012 ilitolewa jana na Hakimu Aniseth Wambura ambapo alisema
mahakama yake imefikia uamuzi huo wa kuitupa rufaa hiyo kwasababu haina
mantiki ya kisheria.
Hakimu Wambura alisema mahakama
yake imekubalina na hukumu iliyotolewa Aprili 2012 na Mahakama ya Mwanzo
Sinza katika kesi ya madai talaka iliyokuwa imefunguliwa na Mshumbusi
anayetetewa na wakili wa kujitegemea Philemon Mutakyamilwa dhidi ya
Maimbo ambapo mahakama hiyo ya chini ilitangaza kuwa hakukuwa na ndoa
baina ya watu hao kwasababu Maimbo alikuwa ni mzinzi, simwaminifu katika
ndoa yake na alikuwa akimtesa mkewe.
“Baada ya mahakama yangu kusikiliza
hoja za mwomba rufaa na mjibu rufaa ,mahakama hii imefikia uamuzi wa
kukubali hoja za Mshumbisi kuwa kwa tabia ile ya mbaya ya uzinzi na
ukosefu wa uaminifu katika ndoa yake hapakuwepo na ndoa baina yao hivyo
mahakama yake inatangaza kuwa hukumu ya mahakama ya Mwanzo Sinza ambayo
iliivunja ndoa hiyo ilikuwa hukumu sahihi “alisema hakimu Wambura.
Akizungumza na mwandishi wa habari
hizi baada ya kutolewa kwa hukumu hiyo wakili Mutakyamilwa alisema
amefurahishwa na hukumu hiyo kwani mahakama imetenda haki kwasababu
kesi hiyo ya madai ya talaka ilikuwa na msukumo wa siasa chafu
zilizokuwa na lengo chafu la kumchafulia jina mteja wake(Mshumbusi)
ambaye kwa sasa ni mzazi mwenzie Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema), Dk.Wilbroad Slaa.
Kutokana na hali ni wzi kwamba Dk Slaa sasa wanaweza kuoana na mpenzi wake huyo waliyezaa naye mtoto mmoja.
No comments:
Post a Comment