|
Sheha aliyemwagiwa tindikali na watu wasiojulikana akiwa hospitalini alipolazwa kwa matibabu |
SHEHA
wa eneo la Tumondo, visiwani Zanzibar, Mohamed Omary Said, amemwagiwa tindikali na mtu asiyejulikana
na hivyo kupata maumivu makali sehemu yake ya kifua na jicho kuumia
pia.
Sheha huyo alikimbizwa katika Hospitali ya Mnazi mmoja mjini Unguja ambapo alipatiwa matibabu ya dharura.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Mukhadam Khamis, amesema
chombo kilichotumika kumwagia tindikali Sheha huyo kilipatikana eneo la
tukio na kwamba polisi imekichukua kwa kukichunguza kitaalam ili
kugundua aliyekuwa akikitumia kwa kuangalia alama za vidole.
Sheha huyo alimwagiwa tindikali jana usiku wakati alipotoka nje ya
nyumba yake kuchota maji na ndipo mhalifu huyo alipomwagia tindikali na
kwamba hakuweza kumtambua.
Miezi michache iliyopita Katibu wa Mufti wa Zanzibar, Sheikh Fadhil Soraga naye alimwagiwa tindikali kabla ya imamu wa msikitini mjini humo kuuwawa kwa kukatwa mapanga sikui chachje baada ya matukio ya viongozi wa Kikristo kupigwa risasi na watu wasiojulikana.
No comments:
Post a Comment