STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, May 27, 2013

Vyama vya ngumi vya TPBO, TPBC vyalumbana

http://dewjiblog.com/wp-content/uploads/2012/09/OnesmoNgowi.jpg
Rais wa TPBC, Onesmo Ngowi


http://www.ippmedia.com/media/picture/large/tpboyassinpresidaaa.jpg
Rais wa TPBO, Yasin Abdallah 'Ustaadh'



MASHIRIKISHO ya ngumi za kulipwa nchini yenye heshima kubwa katika mchezo huo, TPBO na TPBC vimeingia kwenye malumbano kila kimoja kikishutumu na kuanika udhaifu wa wenzake kisa ikiwa ni mahojiano aliyoyafanya bondia nyota wa zamani George 'Lister' Sabuni na gazeti moja la kila siku.
Katika habari hiyo Sabuni alinukuliwa akiliponda Oganaiziesheni ya Ngumi za Kulipwa, TPBO kwamba inawakimbiza mapromota kutokana na kuendeshwa kibabaishaji na kuwataka mabondia wapitia Kamisheni ya Ngumi Tanzania, TPBC analofanya nayo kazi.
Hata hivyo kauli hizo zilimfanya Rais wa TPBO, Yasin Abdallah 'Ustaadh' kuwaka na kuanika madudu ya uongozi wa TPBC, ikiwamo kuwakata mabondia asilimia 10 ya fedha kwa safari zao za nje ya nchi badala ya asilimia 1 na mengine ambayo yalijibiwa na Rais wa TPBC, Onesmop Ngowi.
Ngowi alifafanua taarifa kwamba wao TPBC ndiyo waliosababisha promota maarufu nchini wa zamani wa ngumi, DJB Promoters chini ya Jamal na Dioniz Malinzi kuachana na mabondia Rashid Matumla na Mbwana Matumla akidai mabondia hao waliandika wenye barua baada ya kuhamia kwa Kajumulo na Don King Promotions na siyo kweli kama kamisheni yao inahusika.
Kifupi ni kwamba malumbano hayo kwa wadau wa ngumi hayawasaidii na muhimu viongozi hao ambao kwa siku za karibuni walikuwa wakifanya kazi kwa pamoja kukaa chini na kumaliza tofauti zao kwa manufaa ya mchezo huo.
Huu ni mtazamo wa MICHARAZO kama mdau wa michezo nchini.

No comments:

Post a Comment