Badala yake, Kibaden ambaye pia ni mchezaji nyota wa zamani wa 'Wekundu wa Msimbazi' aliyewahi pia kuandika rekodi kwa kuifikisha fainali ya Kombe la Shirikisho wakati akiifundisha mwaka 1993, amefichua kuwa Kaseja hakuwamo katika orodha ya wachezaji aliokabidhiwa na uongozi wa klabu yake hiyo.
Akizungumza na jana, Kibadeni, alisema wakati akikabidhiwa
majina ya wachezaji wa timu hiyo ili aanze kuwanoa, jina la Kaseja
halikuwamo na hivyo yeye hawezi kulirejesha kwa maamuzi yake binafsi.
"Sijamkata mimi, ila jina lake sikupewa. Hicho ndicho ninacheweza
kukieleza... mambo mengine ni ya ndani ya klabu," alisema Kibaden,
mshambuliaji nyota wa zamani wa timu hiyo aliyerejea kuwafundisha baada
ya kuihama klabu aliyoiongoza msimu uliopita ya Kagera Sugar.
Alisema kwa sasa tayari ameshapata wachezaji 25 atakaokuwa nao
katika msimu ujao wa ligi, huku akiwataja nyota wa kigeni kuwa ni wawili
na wote wanatokea Uganda.
"Kikosi changu hakitazidi nyota 25, na wageni hadi leo (jana) ni
kipa Abel Dhaira na beki Senkoomi (Samuel), mipango mingine ya ndani ni
ya kiufundi. Mazoezi tunayoendelea nayo ni ya kawaida na wengi waliokuja
kujaribiwa hawajanishawishi kuwachukua," aliongeza Kibaden.
Naye Kaseja ambaye aliwahi kusema kitambo kuwa
hahofii kutemwa Simba, alisema kuwa hivi sasa anachofanya ni kuendelea
kujiweka 'fiti' ili atumikie vizuri taifa kwa sababu yeye na wenzake wa
kikosi cha timu ya taifa (Taifa Stars) wana kazi kubwa ya kuhakikisha
kuwa wanashinda katika mechi ijayo dhidi ya Uganda na kujiweka katika
mazingira mazuri ya kufuzu kwa fainali zijazo za kombe la mataifa ya
Afrika kwa wachezaji wa ligi za ndani (CHAN).
"Jamani kuhusiana na Simba siwezi kusema lolote kwa sasa... ila
maisha ni popote," alisema nahodha huyo wa Taifa Stars ambaye wiki
iliyopita alishuhudiwa akiwa katika mazoezi ya timu ya vijana
ya Simba B, akishauriana na kocha msaidizi wa timu hiyo, Amri Said.
Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage hakutaka kueleza wazi suala
la Kaseja na badala yake akasema kuwa hivi sasa, suala la nani asajiliwe
na nani aachwe liko katika mamlaka ya kamati yao ya ufundi
inayoshirikiana na benchi lao la ufundi.
Rage alisema vigezo vya kusajili mchezaji ni muhimu zaidi
kutekelezwa na makocha na kisha kamati ya utendaji itakuwa ya mwisho
kwa lengo la kutoa baraka.
NIPASHE
No comments:
Post a Comment