Mwenyekiti wa CHADEMA Fremaan Mbowe pamoja na mbunge wa Arusha mjini
Godbless Lema leo wamejisalimisha Polisi baada ya jeshi hilo kutangaza linawasaka baada ya vurugu ziliztokea jana mjini Arusha.
Akiongea na waandishi wa habari, Fremaan Mbowe alisema kuwa wao wamejisalimisha kama
polisi walivyosema wanawatafuta na walipofika waliandika maelezo ambapo
alisema kuwa polisi waliwaita kwa mambo mawili, moja likiwa ni kwa
kuwahoji kwanini walifanya mkutano usio wa halali ambapo alisema
kuwa;
"Jambo la kufanya mkutano pasipo kuwa halali sio kweli kwani polisi
walituruhusu tukafanye mkutano katika sehemu hile lakini
kinachotushangaza tumefanya wamekuja kutupiga mabomu na kusema sio wa
halali na kuhusiana na ushahidi msimamo wangu upo pale pale tunao ushahidi
wa kutosha na tunamjua aliyerusha bomu Jumamosi, lakini hatutautaoa hadi Rais atakapounda Tume Huru ya majaji ili wafuatilie
suala hili. Hao ndiyo tutawaonyesha ushahidi huo, lakini siyo Polisi hatuwezi
kuwapa," alisema Mbowe.
Afande Chagonja akiongea na waandishi wa habari
Kwa upande wa Polisi kupitia Kamishna wa Mafunzo na Operesheni za Kijeshi, Paul
Chagonja akiongea na wanahabari alisema waliwahoji wabunge hao na
kuwaomba ushahidi waliokuwa nao kama wanavyodai, lakini waheshimiwa hao hawakutoa ushirikiano.
"Mbowe alisema kuwa ana ushahidi na hata katika vyombo vya habari
ametangaza lakini nashangaa tulivyomuuliza hapa amesema kuwa hana
ushahidi wowote na wala hajawahi kutamka hivyo sasa sisi kwa kuwa kasema
hivyo nitakaa na makachero wangu na tutaangalia jinsi ya kufanya"alisema
Chagonja
Aidha alisema kuwa alimuliza mbunge wa Arusha mjini kwanini awali
alikuja kuwasifia Polisi baadae akawageuka ilihali alishasema katu hawezi kusema uongo na kuwajibu kuwa, yeye anafuata mwenyekiti wake anachosema.
No comments:
Post a Comment