Wahanga wa mlipuko wa jana jijini Arusha |
WATU wawili ambao ni wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema) , waliofariki jana baada ya kulipukiwa na bomu katika mkutano
wa kampeni za uchaguzi wa Udiwani kata ya Kaloleni,jijini Arusha,
mmoja ametambuliwa na mwingine bado hajafahamika.
Mganga, mfawidhi wa hospital ya mkoa wa Arusha, Dakta Josiah Mlay, amemtaja marehemu huyo kuwa ni Judith Mushi, (46) mkazi wa Sokon one jijini Arusha, na mwingine ni kijana wa kiume anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka kati ya 15-16 ambae hajafahamika ambae alifia hospital ya AICC.
Dakta Mlay, amesema katika tukio hilo hospital hiyo imepokea majeruhi 10 kati ya 15 na wote ni wanaume isipokuwa majweruhi mmoja wa kike aitwae Sharifa Jumainne ,ambae hali yake ni mbaya.
Amesema kuwa katika uchunguzi wa awali imegundulika kuna kupande cha chuma kwenye mapafu ambacho kinatokana na mlipuko wa bomu
Aidha amesema kuwa majeruhi mwingine aliyepata majeraha ya kichwa amehamishiwa kwenye hospital ya Seliani ya Arusha kwa uchunguzi zaidi akisubiriwa kupelekwa hospital ya rufani ya KCMC ya mjini Moshi.
Dakta Mlay, amesema hali za majeruhi wengine waliolazwa hospital ya mkoa wa Arusha ya mount Meru, zinaendelea vizuri.
Wakati huo huo tume ya taifa ya uchaguzi jimbo la Arusha, imeahirisha uchaguzi huo hadi June 30 mwaka huu kutokana na tukio hilo la mripuko wa bomu lililojeruhi watu .

Katika hatua nyingine mkuu wa mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo,
amewatembelea majeruhi wa mlipuko huo waliolazwa katika hospital
mbalimbali za mkoani Arusha zikiwemo mount Meru, Seliani, na AICC .
Katika hatua ingine viongozi mbalimbali w a chadema wametembelea katika
eneo la tukio akiwemo mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo
chadema Freeman Mbowe na wabunge wa jimbo la Arumeru pamoja na Arusha
mjini.
Chanzo:Libeneke
No comments:
Post a Comment