WATU 13 wamepoteza maisha na wengine zaidi ya 20 kujeruhiwa vibaya katika matukio mawili ya ajali za barabarani zilizotokea katika mikoa ya Mbeya na Dodoma usiku wa kuamkia leo.
Habari toka Dodoma zinasema watu sita watatu wanaotajwa kuwa na uhusiano wa kidugu wamefariki baada ya basi ya Al Saedy linalofanya safari zake kati ya Dar na Dodoma kugongana uso kwa uso na lori eneo la Chalinze mkoani humo majira ya saa 4 usiku.
Nako Mbeya watu wengine saba nao walipoteza maisha katika ajali mbaya huku watu zaidi ya 10 wakiwaachwa hoi kwa majeraha mabaya katika ajali iliyohusisha daladala aina ya Toyota Hiace kwa kilichoelezwa mwendo kasi na kufeli kwa breki.
Kwa tukio la Dodoma lililotokea usiku wa saa 4 inaelezwa watu waliofariki ni waliokuwa ndani ya lori hilo ambapo wanandugu watatu akiwamo dereva walipoteza maisha papo hapo sambamba na utingo wa gari hilo na wengine ni wale waliokuwa kwenye basi hilo la Al Saedy.
Kwa ajali ya Mbeya wengi wa waliofariki ni abiria wa 'kipanya' na kondakta wake na Kamanda wa Polisi wa mkoa huo, Diwani Athuman amewakumbusha madereva kuwa waangalifu wawapo barabarani.
Ajali hizo zimetokea wakati Tanzania ikiwa ndani wa Wiki ya Nenda kwa Usalama.
Lori la mizigo lililogongana uso
kwa uso na basi la Al - Saedy lililokuwa likitoka Dar Es salaam kuelekea
Mkoani Dodoma jana usiku linavyofanana baada ya kugongana na basi hilo
uso kwa uso
Basi la Al Saedy linavyoonekana
mara baada ya kugongana na lori la Mizigo Maeneo ya Chalinze Mkoani
Dodoma Jana Usiku
Basi
la Al Saedy linavyoonekana mara baada ya kugongana na lori la Mizigo
Uso Kwa Uso jana usiku eneo la Chalinze Mkoani Dodoma.
No comments:
Post a Comment