STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, October 25, 2013

MSAIDIE MTOTO HUYU, MATESO YA MIAKA 11 IMETOSHA KWAKE

Ndivyo mtoto Honolina Cristian anavyoonekana kwa karibu

Kama umejaliwa uwezo kwa nini usitoe kwa mtoto huyu akatibiwe upate Thawabu

Hivi ndivyo mtoto huyu anavyoteseka na madonda

Mtoto akionyesha ulimi ulioota tena baada ya awali kukatwa
HUJAFA Hujaumbika! Mtoto Honolina Christian (11) yupo kwenye mateso makubwa na amewalilia Watanzania wote kuanzia Rais Jakaya Kikwete, serikali yake nzima na wanajamii akiwaomba msaada wa kumwezesha apate matibabu yatakayookoa maisha yake.
Mtoto huyo ambaye huwezi kumuangalia mara mbili bila kutokwa na machozi alisema tumaini lake ni kwa watu watakaoguswa na kilio chake akidai ameteseka vya kutosha na hivyo anadhani umefika muda na yeye afurahie maisha kama watoto wengine.
Akizungumza na MICHARAZO akiwa ameongozana na mama yake, mtoto Honolina alisema maumivu anayopata kwa madonda yanayoitafuna ngozi yake yanamnyima raha na angeomba asaidiwe aweze kwenda kufanyiwa matibabu nje ya nchi ili na yeye apumue.
"Naumia...Nateseka na sijui niseme nini. Nawaomba Watanzania kuanzia Rais, Wabunge, Mawaziri na watu waliojaliwa uwezo wanisaidie niweze kupata matibabu, nimeteseka na ninateseka sana na ugonjwa huuu..." Honolata alisema huku akianza kulia kwa simanzi.
Mama yake mzazi aliyeambatana na mtoto huyo, Grace John alisema tangu mwanaye azaliwa Juni 12, 2002 hajawahi kufurahia maisha kutokana na maradhi yaliyomuandama katika namna ya ajabu kabisa.
"Kwanza alizaliwa akiwa amejaa nywele mwili mzima na baadaye nywele hizo kupukutika kisha mwili mzima kuwa kama ngozi ya chui na kumkimbiza hospitali ya Morogoro alipopewa mafuta ya ngozi kumtibia," alisema.
Mkazi huyo wa mkoani Morogoro, anasema tangu hapo mwanaye amekuwa akiteseka na kuharibika ngozi ikiwemo kuota pembe mbili kichwani na kuwa na ndimi saba zilizofanyiwa upasuaji KCMC kabla ya mapembe hayo kumuacha na mashimo kichwani yaliyolazimisha azibwe kwa ngozi ya pajani.
"Kifupi ni kwamba nimehangaika sana na mwanangu huyu, tangu akiwa mchanga mpaka leo, bahati mbaya ni kwamba baba yake mzazi alifariki mwaka 2007 na kuniachia mzigo ambao kwa hakika nimeuvumilia na kushindwa kujua mwishowe utakuwaje," alisema Grace.
Grace aliongeza alikuja jijini Dar mwezi uliopita kwa ajili ya matibabu ya mtoto wake huyo katika Hospitali ya Muhimbili, lakini aliambiwa arejee nyumbani na mwanaye akielezwa mwanae ni mlemavu wa ngozi mweusi (Albino Mweusi).
"Kama mtoto anavyokueleza, nawaomba wasamaria wema, serikali na watu wenye uwezo watusaidie.. wanichangie nimuokoe mwanangu...miaka 11 ya mateso nadhani inatosha, sitaki kumpoteza mwanangu nampenda katika hali aliyonayo," alisema Grace akilengwalengwa na machozi.
Alisema huyo ni mmoja wa watoto wake watatu aliozaa na mwanaume ambaye bahati mbaya hakufunga naye ndoa kabla ya kufa kwa ajali ya gari wakati wakiendelea kuhangaikia kwa pamoja matibabu ya Honolina.
"Huyu ni mtoto wangu wa kwanza kuzaa na Christian niliyezaa naye watoto watatu, wengine ni Dickson (9) na mwisho aliniacha nikiwa mjamzito wa mimba yake ni Francis (6), ambao wote hawana tatizo kama dada yao," alisema.
Alisema watoto wake hao kwa sasa wanaishi pekee yao Mgeta, Morogoro wakati yeye akihangaika na Honolina apate matibabu, akidokeza pia nyumba aliyokuwa amejenga na 'mumewe' imeuzwa na mama mkwe wake na hivyo kumfanya kuwa na wakati mgumu kwa vile ana pa kuishi na hana shughuli ili kumtibia mwanae.
Aliongeza kwa yeyote atakayeguswa na tatizo la mwanae anaweza kumsaidia kwa kuwasilisha michango yao ama kwa MICHARAZO MITUPU au kupitia simu zake za mkononi kwa huduma za Tigo-Pesa, M-Pesa au Airtel Money kwa namba 0719-749542, 0687-402694 na 0762-425973.
NB:Makala ndefu ya mtoto huyu itawajia baadaye kidogo, unaweza kulia kwa jinsi inavyosikitisha

No comments:

Post a Comment