Na Boniface Wambura
PAMBANO
la Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya wenyeji Ruvu Shooting na Simba
lililochezwa jana (Oktoba 5 mwaka huu) katika Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam imeingiza sh. 75,692,000.
Watazamaji
waliokata tiketi kushuhudia pambano hilo namba 43 la VPL msimu wa
2013/2014 lililomalizika kwa timu hizo kutoka sare ya bao 1-1 walikuwa
13,395.
Viingilio
katika mechi hiyo vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh.
20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 17,983,902.31 wakati Kodi ya
Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 11,546,237.29.
Mgawo
mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 9,144,357.11,
tiketi sh. 3,183,382, gharama za mechi sh. 5,486,614.26, Kamati ya Ligi
sh. 5,486,614.26, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh.
2,743,307.13, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Pwani (COREFA) sh.
1,066,841.66 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA)
sh. 1,066,841.66.
No comments:
Post a Comment