Kipa Juma Kaseja aliyemwaga wino Yanga |
Kwa
mujibu wa kanuni, klabu zenye fursa ya kusajili wachezaji katika
dirisha dogo ni zile ambazo hazijatumia nafasi zote 30 za wachezaji.
Ligi
Kuu ya Vodacom (VPL) na Ligi Daraja la Kwanza (FDL) zimemaliza duru la
kwanza msimu huu. Duru za pili litaanza kutimua vumbi Januari mwakani.
Kwa
mujibu wa Kalenda ya Matukio ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF) matukio ya Novemba na Desemba ni dirisha dogo la usajili na mechi
za kirafiki za Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA)- FIFA
Date.
Matukio
mengine ni michuano ya Kombe la Uhai inayoshirikisha wachezaji wenye
umri chini ya miaka 20 wa klabu za VPL na michuano ya Kombe la Chalenji
itakayofanyika Nairobi, Kenya.
Tayari baadhi ya klabu zimeshaanza kuwekana sawa na wachezaji kwa kuwasainisha mikataba kama ilivyofanya Yanga kwa kipa wa zamani wa Simba, Juma Kaseja aliyemwaga wino kwa kuichezea timu hiyo kwa miaka miwili kwa donge la Sh Mil 40.

No comments:
Post a Comment