Fabregas akifunga mkwaju wake wa penati jana |
Ronaldo akielekea kufunga bao la kwanza la Real Madrid kabla ya kutolewa kwa maumivu |
Barca wakipongezana |
Villa na Garcia wa Atletico Madrid wakishangilia mabao yao ya jana. Kila mmoja kati ya wawili hao alifunga mabao mawili |
WAKATI Real Madrid ikijibu mapigo kwa mahasimu wao Barcelona waliotangulia kushinda mabao 4-0 kwa kuichakaza Almeria kwa magoli 5-0, Atletico Madrid ilifanya kufuru zaidi kwa kutoa kisago cha mabao 7-0 katika Ligi ya Hispania.
Madrid ilipata ushindi huo ugenini kupitia kwa mabao ya Cristiano Ronaldo aliyefunga bao la mapema la dakika ya tatu tu ya mchezo kabla ya kutolewa uwanjani kwa kuumia.
Mabao mengine yalifungwa na Karim
Benzema dakika ya 61 pasi ya Jese Rodriguez
kabla ya Gareth Bale kufunga bao la tatu dakika ya 71, Isco akaongeza la nne na Alvaro Morata akahitimisha karamu ya mabao dakika ya 81.
Mapema Barcelona waliifumua timu ya Grenada kwa mabao 4-0 bila ya kuwa na nyota wake, Lionel Messi aliye majeruhi.
Magoli ya penati ya Andres Iniesta na nahodha wa zamani wa Arsenal, Cesc
Fabregas yaliipa uongozi Barcelona kabla ya kuongeza mengine mawili kupitia kwa Alex Sanchez na Pedro kuifanya Barca iendeleze rekodi ya kushinda mechi mfululizo.
Hata hivyo ni Atletico Madrid walifanya kufuru usiku wa manane wa leo baada ya kuifumua Getafe kwa mabao 7-0 na kuzidi kung'ang'ania katika nafasi ya pili ya msimamo wa La Liga ikifikisha pointi 37,
Raul Garcia na David Villa walifunga mara mbili, huku Diego Costa, Adrian na lile la kujifunga la Lopo lilitosha kuifanya Atletico kuifukizia Barca inayoongoza kwa pointi 40, tatu pungufu na ilizonazo klabu hiyo.
No comments:
Post a Comment