Rais wa TFF, Jamal Malinzi aliyetoa taarifa za Mwenyekiti wa Simba Ismail Aden Rage aitishe mkutano haraka baada ya awali kupiunduliwa na wajumbe wa kamati ya utendaji ya klabu yake akiwa nje ya nchi |
MWENYEKITI wa Simba, Ismail Aden Rage ameagizwa kuitisha Mkutano Mkuu wa Dharura wa klabu ndani ya siku 14 kuanzia sasa.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF) limetoa agizo hilo baada ya kubaini kuwa mgogoro katika klabu
baada ya kupokea barua mbili; moja kutoka Kamati ya Utendaji ikielezea
kumsimamisha uongozi Rage, na nyingine kutoka kwa Mwenyekiti huyo
ikielezea kutotambua kusimamishwa huko.
Uamuzi
wa TFF umefanywa kwa kuzingatia Ibara ya 1(6) ya Katiba ya Simba
inayosema:
“Simba Sports Club ni mwanachama wa TFF, itaheshimu Katiba,
kanuni, maagizo na uamuzi wa TFF na FIFA, na kuhakikisha kuwa
zinaheshimiwa na wanachama wake.”
TFF
itatuma wawakilishi wake katika mkutano huo, na kumuagiza Mwenyekiti wa
Simba kuhakikisha wanachama wote wenye hoja wanapata fursa ya
kusikilizwa.
No comments:
Post a Comment