Oliver Giroud akikosa bao la wazi katika pambano lao la jana dhidi ya Chelsea |
Hekaheka tupu langoni mwa Chelsea, Goroud akikosa tena bao la wazi |
Kudadeki imekuwaje lakini! Kama anasema Goroud wakati akisikitikia kukosa bao |
Lampard na Ozil wakitunishia ubavu katika mechi ya jana |
Torres akijaribu kutumbukiza mpira wavuni bila mafanikio |
Hollaaaa! Lampard anakosa naye bao la wazi |
Eden Hazard akiwatoka mabeki wa Arsenal |
Arsena ilikuwa kileleni kwa muda mrefu hata hivyo imetoka nafasi ya tatu iliyokuwa inashika baada ya matokeo ya mechi za wikiendi na kukaa nafasi ya pili nyuma ya vinara Liverpool wakilingana pointi 36 ila wakitofautiana mabao ya kufunga na kufungwa.
Katika mchezo huo wa usiku wa jana timu zote zilikosa mabao ya wazi na wachezaji kuchezeana kitemi wakati fulani licha ya mwamuzi Mike Dean kudhibiti hali hiyo.
Ligi hiyo inatarajiwa kuendelea siku ya Alhamis kwa michezo kadhaa 10 itakazozikutanisha timu zote 20 zinzoshiriki ligi hiyo ambapo kivumbi kitakuwa kati ya Manchester City dhidi ya Liverpool itakayochezwa uwanja wa Itihad.
Mechi nyingine siku hiyo kwa mujibu wa ratiba ya EPL ni kama ifuatavyo hapo chini;
Hull City vs Manchester United
Aston Villa vs Crystal Palace
Cardiff City vs Southampton
Cardiff City vs Southampton
Chelsea vs Swansea City
Everton vs Sunderland
Newcastle United vs Stoke City
Norwich City vs Fulham
Tottenham Hotspur vs West Bromwich
West Ham United vs Arsenal
Manchester City vs Liverpool
No comments:
Post a Comment