Mchungaji Hanold Camping enzi za uhai wake |
Bango lililokuwa likisisitiza kuwa ifikapo Mei 21, 2011 mwisho wa dunia |
YULE mchungaji, mtunzi na mmiliki wa redio ya Kikristo aliyeleta kizaazaa kwa baadhi ya waumini wake duniani kwa kutangaza kwamba Mei 21, 2011 ingekuwa mwisho wa dunia, Hanold Camping, amefariki wiki iliyopita bila mwenyewe kushuhudia siku hiyo ya mwisho kama alivyowahi kutabiria.
Camping alifariki Desemba 15, 2013 yaani wiki iliyopita tu akiwa na miaka 92 kutokana na kuanguka akiwa nyumbani kwake kabla ya hapo alikuwa akisumbuliwa na kiharusi.
Ingawa kifo chake kimekuwa kimyakimya, lakini ni kwamba Camping anakumbukwa kwa jinsi alivyotabiri KIAMA kutokea Mei 21 na kubandika mabando makubwa katika maeneo mbalimbali duniani ikiwamo Tanzania kupitia kituo chake cha radio cha Family Radio Network.
Baada ya utabiri wake wa Mei kutotokea alisema tukio hilo lingejiri Oktoba 21, 2011 na hakuna kitu kama hicho kilicjotokea mpaka mauti yamemkumba na kuwaacha aliowatabiria wakiendelea kudunda kuthibitisha kuwa hakuna anayejua SIKU wala SAA ila MUNGU Mwenyezi Pekee aliyeumba Mbingu na Ardhi na kila kilichopo ndani yake.
No comments:
Post a Comment