TIMU ya
wanawake chini ya umri wa miaka 20 Tanzania 'Tanzanite' imefungwa mabao
4-1 na Afrika Kusini 'Basetsana' kwenye mchezo wa raundi ya pili ya
kutafuta nafasi ya kufunzu kombe la dunia mwakani nchini Canada kwenye
mchezo uliochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Afrika
Kusini ilianza vyema mchezo huo kwa
kuwazidi ujanja Tanzanite katika
kipindi cha kwanza cha mchezo baada
ya kuzitumia vizuri nafasi walizopata kwa kufunga bao la kwanza dakika ya nne
ya kipindi cha kwanza kupitia kwa mchezaji wake Amogelang Motay.
Bao hilo
liliamsha mashambulizi makali kwa
Tanzanite waliokuwa wakitafuta nafasi ya kusawazisha ambapo dakika ya 13
walifanikiwa kusawazisha kupitia kwa Theresa Yohana alimpiga shuti la mita kama 30 na
kuingia golini moja kwa moja.
Mashambulizi
yaliendelea pande zote mbili, ambapo dakika ya 17 mchezaji wa Afrika Kusini
Shiwe Nogwanya aliipatia timu yake bao la pili lililodumu hadi mapumziko.
Baada ya mapumziko
timu zote zilikuwa zikifanya mashambulizi
lakini Afrika Kusini waliendeleza mashambulizi yao upande wa Tanzanite
na kufanikiwa kupata bao la tatu kupitia kwa mchezaji wake Mosili Makhoali dakika ya 61.
Uzoefu wa Afrika
Kusini ulionekana dhahiri kwani waliliandama lango la Tanzanite kila
mara lakini golikipa Najiat Abbas alikuweza kupangua mashuti kadhaa na
mengine kuishia nje lakini uzembe wa mabeki uliweza kusababisha kufungwa bao la nne dakika ya 78 kupitia
kwa Mosil Makhoali.
Akizungumza baada ya
mchezo kumalizika, Waziri wa habari, vijana michezo na Utamaduni,
Fenella Mukangara aliwataka wachezaji kutolia kwani mwanamke jasiri
anapanga nini afanye baada ya alichotangulia kukifanya hivyo kwa pamoja
na benchi la ufundi wakae watathimini walipokosea ili wafanye
marekebisho kwa ajili ya mchezo wa marudiano
No comments:
Post a Comment