Ashanti United inayoongoza kwa kuomba usajili wa wachezaji 15 katika dirisha dogo |
SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limesema kuwa Pingamizi la wachezaji waliosajiliwa katika dirisha dogo mwisho wake utakuwa Desemba 23 mwaka huu.
Usajili huo uliohusisha klabu za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) na Ligi Daraja la
Kwanza (FDL) ulifanyika kati ya Novemba 15 mpaka Desemba 15 mwaka huu.
Katika
VPL, Kagera Sugar, Mtibwa Sugar na Coastal Union ndiyo timu pekee kati
ya 14 za ligi hiyo ambazo hazikuwasilisha maombi ya usajili katika
dirisha dogo.
Ashanti
United ndiyo inayoongoza kwa wachezaji 15 ambao ni Kassim Kilungo,
Mohamed Banka, Bright Obinna, Victor Costa, Juma Mpongo, Juma Jabu, Ally
Kondo, Shafii Rajab, Mohamed Faki, Abubakar Mtiro, Patrick Mhagama,
Ally Kabunda, Hassan Kabuda, Idd Ally na Rahim Abdallah.
Ruvu
Shooting; Ally Khan na Jumanne Khamis, Rhino Rangers; David Siame, John
Kauzeni, Salum Mamlo, Jingo Seleman, Darlington Enyinna, Rajab Twaha,
Godfrey Mobi na Mussa Digubike. Mbeya City; Saad Kipanga. Tanzania
Prisons; Dennis Liwanda, Godfrey Pastory, Henry Mwalugala, Jamal Salum
na Brayton Mponzi.
Oljoro
JKT; Jacob Masawe, Mansour Ali, Juma Mohamed, Amour Mohamed, Mohamed
Ali, Mussa Nahoda, Benedict Ngasa, Seleman Makame, Shija Mkina, Ali Omar
na Shaweji Yusuf. Simba; Uhuru Selemani, Ivo Mapunda, Ali Badru, Awadh
Juma, Donald Mosoti na Yaw Berko. Azam; Mouhamed Kone.
Yanga;
Hassan Dilunga, Juma Kaseja na Emmanuel Okwi. Mgambo Shooting; Suleiman
Khatib, Bolly Ajali, Amri Sambinga na Issa Ali. JKT Ruvu; Chacha Marwa,
Sino Augustino, Idd Mbaga na Cecil Luambano.
Katika hatua nyingine, Kamati
ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) itakutana
Jumapili (Desemba 23 mwaka huu) chini ya Mwenyekiti wake, Rais Jamal
Malinzi.
Kikao
hicho kitakachofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kitapitia ajenda
mbalimbali ikiwemo uundwaji wa vyombo vya haki (Kamati ya Nidhamu,
Kamati ya Maadili na Kamati ya Uchaguzi).
No comments:
Post a Comment