STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, January 2, 2014

Polisi Arusha katika kashfa, wanakwaya 6 wadaiwa kupigwa bomu na askari

https://fbcdn-sphotos-b-a.akamaihd.net/hphotos-ak-ash4/395583_170893516406261_293707556_n.jpg
Majeruhi wa bomu la Mei 6 kanisa la Mtakatifu Mfanyakazi jijini Arusha
 HABARI ambazo zimeripotiwa muda mfupi uliopita na kituo cha redio cha Wapo kimeeleza kuwa wanakwaya sita wa Kanisa Katoliki mkoani Arusha wamejeruhiwa kwa kilichoelezwa kupigwa bomu na askari wakati wakitoka kanisani usiku wa mkesha wa mwaka mpya.
Inadaiwa wanakwaya hao walikuwa katika makundi na ghafla wakitokea kanisani na kuvamiwa na gari la doria la Polisi na kisha kupigwa na bomu lililowafanya wanguke na kujikuta miili yao ikiwa imechanwachanwa na kulowa damu na kukimbizwa hospitalini na kulazwa huku wengine kuwaliokuwa nao kuruhusiwa kurudi majumbani.
Askofu Lobulu amenukuliwa akisikitishwa na kitendo hicho na kuhoji vipi kanisa katoliki liandamwe na mashambulizi ya mabomu akirejea tukio la Mei 6 kanisa la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi kupigwa bomu na kuua watu kadhaa na kujeruhiwa wengine kibao.
Hata hivyo Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha Liberatus Sabas amesema atatoa ufafanuzi wa tukio hilo kesho kwenye mkutano wa wanahabari, huku akisema anajua ni wanawake wawili tu ndiyo waliojeruhiwa katika tukio ambalo hata hivyo hakupenda kulizungumza kwa kina kwa madai atafanya hivyo kesho.
Tukio hili liemkuja huku jeshi la Polisi likishuhudia likipata IGP mpya Ernest Mangu na naibu wake, Abdulrahman Kaniki, na pia mkoa huo ukiwa kuna matukio ya milipuko ya bomu likiwemo lile la kwenye mkutano wa CHADEMA.
Tusubiri kupona kesho RPC Sabas atuweke sawa juu ya ukweli wa tukio hilo la fungua mwaka 2014.

No comments:

Post a Comment