LIGI
Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, inaingia raundi ya 16 kesho (Februari 5
mwaka huu) kwa mechi tano huku Mtibwa Sugar ikiikaribisha Simba kwenye
Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Kiingilio
katika mechi hiyo ambayo itakuwa ya kwanza kuchezwa kwenye uwanja huo
wenye uwezo wa kuchukua watazamaji 10,000 tangu uanze mzunguko wa pili
wa VPL kitakuwa sh. 5,000. Jonisia Rukyaa kutoka Bukoba ndiye
atakayechezesha mechi hiyo.
Mechi
nyingine za ligi hiyo ni Tanzania Prisons vs Coastal Union (Sokoine,
Mbeya), Mgambo Shooting vs Ruvu Shooting (Mkwakwani, Tanga), Rhino
Rangers vs Oljoro JKT (Ali Hassan Mwinyi, Tabora) na JKT Ruvu vs Ashanti
United (Chamazi, Dar es Salaam).
Wakati
huo huo: Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limesitisha matumizi ya
tiketi za elektroniki kwenye viwanja vyote vyenye huduma hiyo ili kutoa
fursa ya kufanyika tathmini ya kina kabla ya kuendelea tena.
Uamuzi
huo umefikiwa kwa kuzingatia sababu mbalimbali baada ya kikao kati ya
Sekretarieti ya TFF na maofisa wa benki ya CRDB kilichofanyika jana
(Februari 3 mwaka huu) katika ofisi za Shirikisho.
Tathmini
hiyo inafanyika ili kubaini changamoto zilizojitokeza na kuzitafutia
ufumbuzi kabla ya kuendelea tena na matumizi hayo, kubwa ikiwa ni
hadhari iliyotolewa na vyombo vya Usalama juu ya misongamano inayotokea
uwanjani kutokana na kutokuwepo mtiririko mzuri wa uingiaji.
Tayari
zipo changamoto za wazi ikiwemo uelewa wa washabiki wa jinsi ya kununua
na kutumia tiketi hizo, milango michache ya kuingilia uwanjani na
washabiki wengi kununua tiketi dakika za mwisho hivyo kuchangia
misongamano.
No comments:
Post a Comment