Mwenyekiti wa TWFA, Linnah Mhando |
Mwenyekiti wa TWFA, Linnah Mhando amesema shirikisho lake kupitia Kamati ya Wanawake ya mpira wa miguu kwa wanawake, wanatambua umuhimu wa siku ya wanawake duniani.
“Mpira wa miguu kwa wanawake ni moja ya michezo inayokuwa kwa kasi katika bara la Afrika na hata hapa nyumbani. Idadi ya wasichana wanoshiriki katika mpira wa miguu imekuwa ikiongezeka mwaka hadi mwaka.
Katika kusheherekea siku ya wanawake duniani mwaka 2014. Sherehe rasmi zitafanyika katika mkoa wa Tanga
TFF /TWFA wanaamini kuwa ili kuwa na kiwango kizuri na maendeleo katika mpira wa miguu wanawake ni lazima kuanza na vijana wadogo hivyo basi Shirikisho na chama cha mpira wa miguu Tanga limeandaa mafunzo kwa walimu wapatao 30 toka shule15 za mkoa wa Tanga.
Walimu hao watapatiwa mafunzo kwa siku mbili na tarehe 08/03/2014 kutakuwa na Tamasha la Grassroot litakalojumusha jumla ya wanafunzi wapatao 1000 toka shule husika.
Ni matumaini ya shirikisho kuwa mafunzo hayo na tamasha la grassroot litaleta mwamko wa mpira wa miguu katika mkoa wa Tanga na hamasa kwa watoto wa kike,wasichana na kina mama katika ushiriki wa mpira wa miguu wanawake.
No comments:
Post a Comment