KLABU
ya Yanga imeingia makubaliano ya kununua nyumba za Shirika la Hifadhi
ya Jamii (NSSF), kwa ajili ya wachezaji wake kupitia program maalumu.
Akizungumza katika hafla ya utiaji saini
makubalinao hayo iliyofanyika jana katika Hoteli ya Serena, Mkurugenzi
wa Huduma na Uendeshaji wa NSSF, Crecentius Magori alisema wachezaji
wanapaswa kuona fahari kumiliki nyuma au ardhi mjini, si magari.
Magori alitumia fursa hiyo kuwahamasisha wachezaji wa Yanga ambao
walikuwepo katika utiaji wa saini makubaliano hayo, kuchangamkia mradi
huo uliopo makao mapya katika Kijiji cha Dege, Kigamboni, jijini Dar es
Salaam.
“Sisi tuko tayari
kuwapa fomu na kwenda kuwaonyesha nyumba hizo za kisasa zaidi, hivyo
ningependa kuwashauri mpatapo fedha za mikataba, mkitoa kiasi nanyi muwe
wamiliki wa nyumba hizo. “Kama utamudu na kutoa kiasi cha sh. mil.8 na
kulipa kwa miezi mitatu mfululizo, NSSF watawapa ufunguo na kuendelea
kulipa kila mwisho wa mwezi kwa miaka 15, kisha unakuwa mmiliki halali
wa nyumba hiyo,” alisema Magori. Aliongeza kuwa hata ikitokea mchezaji
akafariki dunia, nyumba hiyo itaendelea kuwa mali ya familia ya mhusika
kwani itakuwa imerithiwa huku akisihi wachezaji ambao si wanachama wa
NSSF, kujiunga ili kupata manufaa ya shirika hilo. Akizungumza katika
hafla hiyo, Katibu Mkuu wa Yanga, Beno Njovu, alisema makubaliano hayo
ni matokeo ya mazungumzo kati ya Mwenyekiti wa klabu hiyo, Yusuf Manji
na Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dk. Ramadhan Dau.
Alisema lengo ni
kuhakikisha kila mchezaji wa timu hiyo anawezeshwa kumiliki nyumba ikiwa
ni moja ya mali ya kudumu ambayo itakuwa na manufaa yake wakati
anacheza, hata baada ya kustaafu soka
KATIBU MKUU WA YANGA, BENO NJOVU, ALIKUWEPO. |
MAXIMO, MSAIDIZI WAKE LEIVA, SALVATORY EDWARD WAKISIKILIZA KWA UMAKINI MKUBWA. |
MPOGOLO NA JACOB, WALIKUWEPO. |
BAADHI YA MIJENGO. |
PICHA KWA HISANI YA SALEHJEMBE.CM
No comments:
Post a Comment