Jumla
ya vikongwe 38 wameuawa mkoani Shinyanga katika matukio tofauti,
yakiwamo ya kuhusishwa na uchawi na ushirikina na wengine kudaiwa
kutowapa urithi watoto wao matokeo yake watoto kuua wazee wao
Akizungumza
na waandishi wa habari juzi kamanda wa jeshi la polisi mkoani Shinyanga
SACP Justus Kamugisha,alisema vikongwe wamekuwa wakiuawa, bila ya kuwa
na hatia kutokana na kuhisiwa kuwa ni wachawi.
Alisema
mbali na imani za kishirikina vikongwe wengine wamekuwa wakiuawa
kikatili wakidaiwa kung’ang’ania mali na kutowagawia watoto wao hivyo
watoto hao kuamua kutekeleza mauaji hayo.
Kamugisha
alifafanua katika kipindi cha mwezi Januari hadi Desemba mwaka jana
(2013), jumla ya vikongwe 27 wameuawa yaani katika halmashauri ya wilaya
ya Shinyanga vijijini vikongwe 11, Kahama 9 na Kishapu 7.
Aliongeza
kuwa katika kipindi cha mwezi Januari hadi Julai mwaka huu
(2014),vikongwe 11 wameuawa,ikiwa katika halmashauri ya wilaya ya
Shinyanga vijijini vikongwe 6, Kahama 4, Kishapu mmoja.
“Jumla kuu ya vikongwe waliouawa katika kipindi cha mwaka jana hadi Julai mwaka huu wa 2014,ni 38”,alisema kamanda Kamugisha
Kufuatia
mauaji hayo kamanda Kamugisha aliwataka wakazi wa mkoa wa Shinyanga
kuacha kuendekeza imani za kishirikina,ambazo zimekuwa zikichangia kwa
kiasi kikubwa mauaji hayo ya vikongwe, huku akiwataka vijana
kushighulisha ili kujipatia kipato na kuacha dhana tegemezi ya mirathi.
Kamugisha
alisema katika msimu wa mwaka huu wa mwaka 2014/2015, atahakikisha
anakomesha uhalifu mkoani Shinyanga, pamoja na kutokomeza mauaji hayo ya
vikongwe na watu wenye ulemavu wa ngozi (albino).
Aidha
aliwataka wananchi likiwamo na jeshi la jadi sungu sungu kushirikiana
kwa pamoja na kuhakikisha, wanawakamata wahalifu, ili kuwafikisha
katika vyombo vya dola, na kuchukuliwa hatua kali za kisheria ili
liwefundisho kwa watu wengine.
Aliongeza
kuwa hivi sasa anatarajia kusambaza polisi kata, kwa kila kata kwani
baadhi ya kata hazina polisi hao, hali ambayo itasaidia kushirikiana kwa
ukaribu na wananchi katika kuhakikisha anawatia nguvuni waharifu.
No comments:
Post a Comment