Bondia Thomas Mashali katikati
akisaini mkataba wa kucheza na Henry Wandera kutoka Kenya Novemba 4
katika ukumbi wa New Madiba 'Korini' uliopo Tandale Dar es salaam. Wanaoshudia kushoto ni Rais wa Oganaizesheni ya Ngumi za kulipwa nchini
TPBO, Yassini Abdallah 'Ustaadh' na promota wa mpambano huo Khamis Ally.
Rais wa TPBO Yassin Abdallah akirekebisha mkataba wa bondia Thomas Mashali katikati atakayepambana na mkenya Henry
Wandera Novemba 4 katika ukumbi wa New Madiba 'Korini' uliopo Tandale
Dar
es salaam kulia ni promota wa mpambano
huo Khamis Ally
Bondia Thomas Mashali katikati akiwe Dole Gumba katika mkataba wa kucheza na Henry Wandera kutoka Kenya Novemba 4. |
****
BONDIA Thomas Mashali 'Simba
Asiyefugika' anatarajia kupanda tena ulingoni Novemba 4 kumvaa Mkenya Henry Wandera katika pambano litakalofanyika katika ukumbi wa New Madiba
zamani Korini.
Mashali anapigana akiwa na
historia ya kupoteza mpambano wake wa mwisho zaidi ya bondia Mada Maugo
ambapo walicheza katika uwanja wa taifa na kupoteza kwa pointi mpambano
huo.
Akizungumzia mpambano huo Mashali
amesema hatokubali kupoteza tena mchezo huo ukizingatia anachezea
nyumbani mahali alipozaliwa na ndipo alipoanzia ngumi maeneo ya Tandale.
"Sintokubali niaibike mbele ya ndugu zangu hivyo nawaambia wapenzi
waje kwa wingi kuangalia Mashali anavyofanya kazi yake ya mchezo wa
masumbwi.
Naye promota wa mpambano huo Khamis
Ally amewahakikishia kuwa sehemu ya kuegeshea magari ni kubwa na ulinzi ni wa
kutosha kifupi katika ulinzi tumejipanga vizuri pia siku hiyo kutakuwa
na mapambano mengine mazuri ya utangulizi ambapo mabondia wengi
wamejitokeza kucheza siku hiyo.
Siku hiyo pia kutakuwa na uuzwaji wa DVD ambazo zinatoa mwanga kwa
mchezaji kujua mchezo na kufahamu zaidi mbinu mpya zitumiwazo na mataifa
mbali mbali Duniani.
Wakiwemo mabondia bingwa wa dunia kama
Manny Pacquaio, Floyd Maywether, Amir Khan, Muhammed Ali, Mike 'Iron' Tyson na
wengine wengi wanaotamba na waliotamba katika mchezo huo wa masumbwi
Duniani.
Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa ngumi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' ametoa wito kwa makampuni
mbalimbali kujitokeza kutoa sapoti ya mchezo wa masumbwi kwani ndio
mchezo pekee unaoweza kututoa kimasomaso watanzania tukafurahi.
No comments:
Post a Comment