STRIKA
USILIKOSE
Sunday, August 3, 2014
'Ningeshangaa kama Yanga isingeenda Kagame'
KOCHA za zamani wa klabu ya Yanga, Kennedy Mwaisabula amesema angeishangaa sana Yanga kama isingekubali kwenda kushiriki michuano ya Kombe la Kagame ambayo inatarajiwa katikati ya wiki.
Mwaisabula alisema michuano hiyo ina faida kubwa kwa Yanga hivyo kama isingeenda Kigali-Rwanda kuishiriki angeiona timu ya ajabu.
Kocha huyo alisema alibaki njia panda juu ya tetesi zilizokuwa zikidai kuwa, Yanga isingeenda Kigali kwa vile haikuwa imepewa taarifa kutoka Shirikisho la Soka la Afrika Mashariki na Kati (CECAFA).
Alisema kama Yanga itaitumia vyema michuano ya Kagame itawasaidia kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara ambayo ilisogezwa mbele kwa ajili yao ili ishiriki vyema michuano hiyo.
"Yanga ipo chini ya kocha mpya, Marcio Maximo na ina wachezaji kadhaa wapya ilikuwa ina haki zaidi ya kushiriki michuano hiyo kuliko msimamo wao wa awali," alisema.
Alisema hata hivyo amefurahishwa na maamuzi ya mwisho yaliyotolewa na uongozi wa Yanga kuhusu kwenda Kigali akiamini itakuwa kipimo kizuri kwa kocha na Wabrazil, Andrey Coutinho na Genilson Santos ‘Jaja’ .
Yanga iliyopangwa kundi A na timu za Rayon Sport ya Rwanda, KMKM ya Zanzibar na Atlabara ya Sudani Kusini itaanza kibarua cha kuwania taji hilo iliyotwaa mara tano kuumana na wenyeji Rayon.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment