Frank Mvungi-Maelezo
Serikali
kutumia Euro Milioni 16 katika ujenzi wa Kiwanda cha kuzalisha viuadudu
vinavyoua viluwiluwi vya mbu wanaoambukiza malaria ulioko chini ya
shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) unaotarajiwa kukamilika mwishoni mwa
mwaka huu.
Hayo
yamesemwa na Meneja Uhusiano wa Shirika hilo Bw. Abel Ngapemba wakati
wa mkutano nawaandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.
“Hivi
sasa majengo yote yamekwisha kamilika katika eneo la Maili moja Kibaha
Mkoani Pwani na mitambo yote imeshawasili na wataalamu wanaifunga ambapo
kabla ya mwisho wa mwaka uzalishaji wa majaribio utaanza” Alisema Ngapemba.
Akifafanua zaidi Ngapemba alisema kiwanda hicho kitasaidia kuzalisha ajira za moja kwa moja zipatazo 172 kwa watanzania.
Pia
Ngapemba alibainisha kuwa kiwanda hicho kitakuwa na uwezo wa kuzalisha
lita milioni sita za viadudu kwa mwaka ambapo asilimia 80 ya dawa hizo
zitatumika nchini na asilimia 20 zitauzwa nchi za nje ambazo tayari
zimeonyesha nia ya kuzitaka dawa hizo.
Viadudu
hivyo vinatengenezwa kutokana na vimelea ambao wanakuzwa kwa kutumia
viinilishe mbalimbali na kunyinyiziwa katika maeneo yenye mazalia ya mbu
ambapo viluwiluwi wa mbu wanapovila wanakufa
Kulingana
na ripoti ya upembuzi yakinifu wa mradi huu uliofanywa na NDC kwa
kushirikiana na kampuni ya Labiofam ya Cuba mwaka 2010, mbali na malaria
kusababisha vifo vya Watanzania wapatao 80,000 kwa mwaka,ambapo watu
milioni 18 huugua ugonjwa huo kila mwaka ambapo Serikali imekuwa
ikitumia kiasi cha dola za marekani zipatazo milioni 240 kwa mwaka
katika kupambana na ugonjwa huu.
Ujenzi
wa Kiwanda hicho ulianza miaka miwili iliyopita na kuwekwa jiwe la
msingi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk.Jakaya Mrisho
Kikwete October mwaka 2013 lengo likiwa kupambana na hatimaye kutokomeza
mbu wanaoeneza malaria na magonjwa mengine yaenezwayo na mbu.
No comments:
Post a Comment